Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga na kamati ya amani Mkoa wa Songwe wakiongozwa na mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Songwe Hussen Issa Batunza, walipotembelea ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Juni 01, 2024 kwa ajili ya kufanya mazungumzo mafupi yenye lengo la kuendeleza ushirikiano.
Jeshi la Polisi limekuwa na ushirikiano na taasisi mbalimbali ambazo ni wadau wa usalama kwa lengo la kuelimisha jamii na kukemea matendo maovu ikiwa ni pamoja na vitendo vya ukatili wa kijinsia ili jamii iwe salama.
0 Comments