Header Ads Widget

RC, SERUKAMBA AZUNGUMZA NA WAMILIKI WA SHULE BINAFSI MKOANI IRINGA

   MKUU WA MKOA WA IRINGA PETER SERUKAMBA

Wamiliki wa shule binafsi mkoani Iringa wamelalamikia kutozwa  michango mingi kutoka serikalini jambo ambalo linalohatarisha ustawi wa shule hizo.


Wamesema hayo leo, wakati wa kikao cha wamiliki wa shule binafsi na mkuu wa mkoa wa Iringa, Peter Serukamba.


Wameitaja michango inayokwamisha ukuaji wa shule hizo, kuwa ni kodi za leseni, Ardhi na Jengo, mchango wa mwenge, Mitihani pamoja na michango mingine ambayo imekuwa ikitozwa na serikali kila mwaka na kupelekea changamoto ya uendeshaji wa shule hizo mkoani hapo kutokana na uwezo wao wa fedha kuwqa mdogo.


Aidha, wamiliki hao, wamelalamikia swala la kukamatwa na kufungiwa vituo vya polisi kwa zaidi ya saa 8, kisa madai ya leseni ambayo ni shilingi laki 3, hivyo kumuomba Mkuu wa mkoa, kusaidi utatuzi wa jambo na kutaka busara itumike kwa serikali na mamlaka zake wakati wanapokwenda kukusanya fedha hizo.


 Akimjibu hoja hizo, mkuu wa mkoa wa Iringa, Peter Serukamba amewahakikishia wamiliki hao, kutokukamatwa tena ama kufungiwa katika vituo vya polisi, kisa deni la leseni, huku akiwakumbusha viongozi wa umoja wa wamiliki wa shule binafsi mkoa wa Iringa, kupeleka malalamiko mengine kwa uongozi wa juu zaidi akiwemo waziri wa elimu na katibu wa wizara hiyo.


Pia, amewakumbusha wamiliki wa shule binafsi mkoa wa Iringa, kuwa shule hizo ni biashara na siyo vinginevyo hivyo wanatakiwa wajue namna Bora ya kuendesha shule hizo, pamoja na kuendelea kulipa kodi kama sheria zinavyoagiza.


Rc, Serukamba amewaagiza watendaji wote wanaohusika na ukusanyaji wa kodi na tozo mbalimbali kwa shule binafsi kuhakikisha wanakaa pamoja ili kuweka mikakati ya ukusanyaji wa kodi hizo bila kuathiri utendaji wa pande zote mbili.


Hata hivyo, wamiliki hao kwa pamoja wamezimia kutuma wawakilishi mkoani Dodoma ili kufikisha kilio chao kwa wizara ya elimu.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI