ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Joseph Mafuru ametenguliwa katika nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Mawasilino-Ikulu, nafasi ya Mafuru imechukuliwa na Bw. Addo Missama, ambaye kabla ya uteuzi huo, alikuwa Ofisa mwandaizi, Ofisi ya Rais-Ikulu.
Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Bw. Mafuru ambaye uteuzi wake umetenguliwa, aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma
.
0 Comments