Header Ads Widget

POLISI KILIMANJARO WATUMIA MABOMU YA MACHOZI KUTAWANYA RAIA BAADA YA AJALI YA GARI LA MAFUTA

 

Askari polisi wakitumia mabomu ya machozi kutawanya raia picha hii ya mtandaoni  haihusiani na habari hii

NA MATUKIO DAIMA APP 

ESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limelazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya Wananchi zaidi ya mia sita (600) waliokuwa wamevamia lori lilokuwa limebeba mafuta ya kula aina ya korie lililopata ajali eneo la Njoro wilaya ya Same.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, SACP Simon Maigwa alisema kuwa tukio hilo limetokea Juni 14 mwaka huu ambapo gari lenye namba za usajili T783 CTC aina ya HOWO na trela yake namba T.889 CSK likitokea Dar es salaam kuelekea Arusha liliacha barabara na kupinduka na kusababisha uharibifu wa gari hilo.


Gari lililokuwa limebeba mafuta ya kula likiwa limeanguka wilayani Same mkoani Kilimanjaro na kupelekea polisi kufyatua mabomu ya machozi kutawanya raia waliokuwa wakiiba mafuta 

Alisema kuwa baada ya ajali hiyo kutokea taarifa zilifika kituo cha Polisi na askari waliwahi katika eneo hilo ambapo waliwakuta Wananchi wamevamia gari hilo kwa lengo la kupora mafuta hayo pamoja na jitihada zingine zilizochukuliwa kuwazuia wasiendelee kupora ililazimika Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya katika eneo hilo.

Katika tukio Hilo askari mmoja alijeruhiwa kwa kupigwa na kitu butu (jiwe) kichwani na mwananchi aliyekuwa akipinga amri ya kutawanyika eneo hilo.


Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limetoa wito kwa Wananchi kuacha tabia ya kukimbilia kwenye eneo ambalo ajali imetokea kwa lengo la kufanya uporaji.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI