Benki ya NMB tawi la Nachingwea imekabidhi kompyuta tatu kwa uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa kwa watumishi.
Akizungumza kwenye kikao na watumishi wa Halmashauri ya Nachingwea Meneja wa Benki ya NMB,Saad Masawila alisema kuwa wamekabidhi kompyuta hizo kwa lengo la kuendeleza mahusiano mazuri waliyonayo kati ya Benki na uongozi wa Halmashauri hiyo.
Masawila aliongeza kwa kusema kuwa benki hiyo imekuwa kinara wa ulipaji kodi ya zaidi ya milioni 9 kwa Halmashauri ya Nachingwea kwa kuchangia maendeleo ya wananchi wa wilaya hiyo.
Masawila alisema kuwa wamekuwa wakipewa namba ya malipo kila baada ya miezi mitatu na wanalipa kwa wakati ili kufanikisha shughuli za kimaendeleo katika Halmashauri hiyo.
Aliongeza kuwa wamekuwa wanarudisha faida kwa wananchi kwa kuchangia zaidi ya milioni 50 kila mwaka wa fedha kwa kufanya shughuli mbalimbali katika Halmashauri hiyo.
Masawila alisema kuwa Benki hiyo ina fedha nyingi za utunzaji wa mazingira hivyo namna gani uongozi wa Halmashauri hiyo wamejipanga kuandika andiko ambalo litasababisha wapate fedha hizo.
Alimalizia kwa kuwapongeza watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea kwa kufanya kazi kwa ushirikiano hadi kupata hati safi kwa miaka sita mfululizo sio jambo dogo kabisa.
0 Comments