Header Ads Widget

MWENGE WAIPONGEZA MTUWASA JENZI WA TANKI LA LITA 500,000 MANG’AMBA



Na Mwandishi wetu, Matukio Daimaapp


Kiongozi wa Mbio Za Mwenge Kitaifa Godfrey Eliakimu Mnzava  amezindua mradi wa maji manispaa ya mtwara mikindani mradi unaoenda kunufaisha wananchi 42,0000 wenye thamani ya zaidiya shilingi 588,469,723.50. 


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo kiongozi huyo amesema kuwa ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo baada ya kutembelea na kupitia nyaraka na matumizi ya fedha.


Amesema kuwa mradi huo umekamilika kwa asilimia 100 kwa sasa ambapo tayari wannachi wameza kunufaika na mradi huo ambao kwa muda mrefu ulikuwa unasubiriwa na wananchi.


“Serikali imeelekeza manunuzi yote ya umma yafanyike kupitia mfumo wa kidigitali wa manunuzi ya umma ambao unasimamiwa na mamlaka ya ununuzi ya umma kwa maana ya PPRA.


“Zabuni zote zinatakiwa zipitie katika mfumo wa kidigitali ambapo awali tulikuwa na TANEPS na sasa tuna NEST katika mfumo huo namna ulivyotengenezwa mzabuni anaomba zabuni moja kwa  moja anaweza kuomba zabuni kidigitali  ambapo utachakata na kuchukua mwenye sifa ambao unaedna kupunguza malalamiko” amesema Mnzava



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira MTUWASA Rejea Ng’ondya amesema kuwa mradi huo utanufaisha wananchi wa  maeneo ya Mangamba,  Mtawanya,  uwanja wa ndege pamoja na Mbae ambapo zaidi ya wananchi 42,000 watanufaika.

Katika mradi huu unaosimamiwa na  MTUWASA na kutekelezwa na  mkandarasi Bison Engineering  Company Limited  ambapo ulisainiwa Septemba, 2022  na kukamilika Julai,2023 ambapo kwasa uko kwa asilimia 100 na umeshaanza kutoa huduma kwa wananchi ambapo wenye kipato cha chini wamesogezewa huduma hiyo.


“Mradi huu umeboresha na kuongeza kasi ya upatikanaji wa maji na kuboresha huduma za maji safi na salama ambapo yatapunguza changamoto mbalimbali ikiwemo magojwa ya milipuko” amesema Ng’ondya

  

Nae Mbunge wa Mtwara Mjini Hassan Mtenga amesema kuwa mradi huo unaenda kumaliza tatizo la maji katika maeneo hayo ambayo kwa kiasi kikubwa. 


Amesema kuwa mgao huo ulikuwa ukiathiri wananchi wa mitaa hiyo ambapo kutokana na mazingira wanayoishi ilikuwa changamoto kubwa kwao. 


“Ni kweli tulikuwa na changamoto na uhaba wa maji  licha ya mgao hata maji hayakuwa masafi lakini sasa kukamilika kwa mradi huu tanki la lita 500,000 pamoja na mradi wa chujio tumepiga hatua kubwa na tunaendelea na uboreshaji wa mabomba ya zamani na kuleta mabomba mapya” amesema Mtenga  



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI