Header Ads Widget

MBUNGE ZUENA AKABIDHI SIMU JANJA ZA KUSAJILIA WANACHAMA UWT KILIMANJARO.

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 


MBUNGE wa viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri amegawa simu janja kwa Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) wilaya saba za mkoa kwa lengo la kuzitumia kufanya usajili wa wanachama.



Aidha Mbunge huyo pia amekabidhi kadi 1000 za UWT lengo likiwa ni kuhamasisha wanawake kujiunga na Umoja huo lengo likiwa ni kuimarisha Chama na Jumuiya zake.


Akikabidhi simu na kadi hizo katika ofisi ya UWT Mkoa, Zuena alisema kuwa serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa ambazo zilikuwa ni kipaombele kwa wananchi. 



Alisema kuwa, kutokana na kazi hizo wananchi wanajukumu la kumlipa asante Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumpa kura za kishindo wagombea wanaotokana na CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na kumpa yeye kura za kishindo uchaguzi Mkuu 2025.


Mbunge huyo alikabidhi vitendea kazi hivyo mbele ya Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kilimanjaro, Elizabeth Minde, Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Messe Mollel, Katibu UWT Mkoa, Erimina na Mjumbe wa Baraza la UWT Taifa, Regina Chonjo pamoja na Makatibu wa UWT Wilaya.



MWISHO.. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI