Header Ads Widget

MSIGWA APINGA MATOKEO YA UCHAGUZI CHADEMA KANDA YA NYASA

NA MATUKIO DAIMA APP

ALIYEKUWA mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa, Mch Peter Simon Msigwa, amekukata rufaa kupinga Matokeo ya  uchaguzi uliompa ushindi  Joseph Mbilinyi (SUGU) kwa madai kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni za katiba katika upigaji kura pamoja na kufanyika kwa fujo ambazo zilichangia kuharibu uchaguzi huo.

Msigwa alisema  katika uchaguzi huo kulikuwa na mambo mengi ambayo ni kinyume na uchaguzi za chama cha hicho ikiwa ni pamoja na wapiga kura kuitwa nje  kushawishiwa kumchagua Sugu kwa madai ni maelekezo kutoka kwa mwenyekiti wa chama hicho Taifa Freeman Mbowe.


Msigwa alisema hayo leo  wakati akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Kihesa Kilolo mjini Iringa  kuwa kama chama hicho kitashindwa kufanyia kazi barua yake ya kukata rufaa kitashindwa kujitofautisha na chama cha mapinduzi (CCM) katika swala la uminyaji wa demokrasia na haki.


Katika hatua nyingine Msigwa amekishauri chama hicho kijitafakari upya na kurudi katika misingi yake ya haki na demokrasia kwa kuheshimu mawazo ya watu wote wakiwemo wanachama wao bila kuwapinga na kuwapuuza kwani kupishana kwa hoja ndiyo ukomavu wa kisiasa.



Aidha amekanusha madai ya yeye kuhama chadema na kusema kuwa kamwe hawezi kuhama chama hicho na kwamba ataendelea kupambana ndani ya chama hicho huku akiwaambia wale wote waliokuwa wanatarajia atatangaza kuahama chama hicho wataondoka wao na kumuacha yeye.


Katiba ya CHADEMA inafafanua vizuri wanaopaswa kupiga kura, makatibu wa yale mabaraza baada ya kupiga kura maana yake mwenyekiti wa vijana, mwenyekiti wa wanawake na mwenyekiti wa wazee wana makatibu.

 Waliosimamia uchaguzi huu waliwazuia makatibu kupiga kura kinyume na katiba, kwa hiyo nimekata rufaa kwenye chama changu kwamba hao ambao walipaswa kupiga kura ambao ni makatibu walizuiliwa kupiga kura, makatibu watatu wa mabaraza, kwa hiyo ukiangalia kura zilizongezeka za kwangu zilikuwa sita, watatu hawakuruhusiwa kupiga kura.

 Mmoja wakawa wamemhujumu wa upande mwingine ambaye hakushinda. Kwa hiyo nimekata rufaa kwa chama changu kwamba ushindi ule haukuwa halali na kulikuwa na mbinu chafu"


"Kama nilivyosema mwanzoni nililalamika mmoja wa wasimamizi walau hata angeondoka apishe, kama CHADEMA tunalalamikia CCM, tunalalamikia serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwamba wasimamizi wa uchaguzi huwa hawatendi haki, CHADEMA tulitakiwa tuwe mfano wa kuigwa kwamba katika chaguzi wanaosimamia wanatenda haki, sasa kama mimi mjumbe wa kamati kuu ninatoa malalamiko haya halafu hayasikilizwi tena ndani ya chama cha CHADEMA chenye kutenda haki nani atasikilizwa katika nchi yetu? Kwa hiyo watatu hawakuruhusiwa kupiga kura.

 Kama vile haitoshi wale walioleta fujo wakati wa mchakato wa mwanzo wa kupiga kura wanadai watu wengine hawakuingia ukumbini walianza kuleta fujo mbele ya msimamizi Benson Kigaila wakawa wanaleta fujo 'wanatumika', msimamizi wa uchaguzi Benson


Huku  Benson Kigaila hakuchukua hatua yoyote kama vile ambavyo hakuchukua hatua yoyote kule Njombe kwa wale waliofanya fujo. 


Hali ile inaleta shida na mashaka na harufu ya uvundo ya ukiukwaji mkubwa wa haki ndani ya chama chetu" Mchungaji Msigwa.


Baadhi ya wanachama wa CHADEMA Iringa akiwemo Kabambe Temihanga alimtaka mchungaji Peter Msigwa kutulia na kumwacha Sugu kufanya kazi ya kujenga Chama hicho kwani malalamiko haya iwapo angeshinda yeye ingekuwaje.

Pia alisema rafu za Uchaguzi huo zilianza toka chaguzi wa ngazi za chini na yeye akiwa mwenyekiti wa kanda ila maumivu ambayo wanachama wa chini wamepata ndio ambayo yamemrudia mwenyewe.
MWISHO 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI