Header Ads Widget

"MJANE ATAPELIWA NYUMBA YAUZWA MILIONI 21 TABORA, RMO,MATRONI KITETE LAWAMANI"


Fatuma Materu(34) Mhanga wa kutapeliwa .

Na Fredrick Siwale - Matukio Daima APP TABORA.                           

MJANE mmoja amedaiwa kutapeliwa fedha za upatu na mtumishi wa Serikali na kusababisha nyumba yake kuuzwa kwa mnada, na kupelekea lawama kwa Mganga mkuu wa Mkoa na Matroni Tabora.


Mjane Fatuma Materu (34) mkazi wa mtaa wa Lipuli ,Kata ya Mwalizani katika 

Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, ameiambia Matukio Daima mkoani Tabora.


Bi.Fatuma alisema katika tukio hilo kuna mtumishi wa Serikali kata ya Mwalizani na mtumishi wa Idara ya afya Hospitali ya Kitete  walimuomba Mhanga awaazime sh.milioni 54.5 ili wakazionye  katika kikundi kwa makubaliano ya kuzirudisha pamoja na riba ya sh.milioni mbili .                                 


" Mwandishi nilifanya hivyo kwa imani maana huyo Afisa mtendaji kata ni rafiki yangu na nimekuwa nikimuazima fedha kwa mtindo huo huku akiniaminisha kuwa mtumishi idara ya afya ni rafiki yake na mwaminifu jambo ambalo halikuwa hivyo nakajikuta nimepigwa" Alisema Fatuma.                      nimelipwa kiasi kidogo kwani fedha hizo zilikuwa za biashara ndogo ndogo na nyingine nilikopea kwa marafiki zabgu ili nipate faida ya sh.milioni 2 katika mzunguko huo,Aliongeza Fatuma.


Alisema bila kutarajia alijikuta akianza kudaiwa fedha alizoazima kwa rafiki zake na kupelekea kukamatwa na kushitakiwa ambapo alikiri kuchukua fedha hizo ambazo ilionyesha kuwa ametapeliwa.                   


"Nirikili na dalali kuja kuiuza nyumba yangu kwa gharama ya sh.21 milioni ambapo sh.19 milioni zililipwa deni kwa wadai na dalali alichukua sh.milioni 2 na jikuta naanza kuishi nyumba za kusaidiwa na Wasamalia wema mimi na Watoto wangu watatu" Alilia kwa uchungu Fatuma.


Baada ya nyumba kuuzwa Fatuma anadai kuwa ilibidi apige hodi kwa Mh.Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Batrida Buriani kabla hajahamishiwa mkoani Tanga na kumuomba amsaidie fedha za kujikimu na kulipia mahitaji ya Wanafunzi kiasi cha sh.700,000 (laki saba) ambazo alipewa kama msaada.                            


Bi.Fatuma alisema aliendelea kupambania kulipwa fedha alizotapeliwa bila mafanikio na ndipo inadaiwa alipaza sauti yake katika mkutano wa hadhara wa aliyekuwa Katibu Mwenezi wa siasa itikadi na mafunzo Taifa Paul Christian Makonda na kusikilizwa na maelekezo kutolewa Fatuma arudishiwe fedha zake.                       


"Mwandishi wa habari niliponzwa kwenda kwa Makonda baada ya hapo sikusikilizwa tena kwa kuambiwa " nenda kwa Makonda akakulipe si ulijipendekeza" Alisema Fatuma huku akibubujika  machozi ya uchungu.     


Alisema aliamua kurudi kwenye Uongozi wa hospitali ya mkoa ya Kitete kupiga magoti ili kuinusuru familia yake  ya Watoto Yatima ambapo anadai kuwa Mganga mkuu wa mkoa Dr.Waziri Mark kwa kushirikiana na Matron Bi.Mwanaidi Shange walimlipa sh.  milioni 4 na kuahidi kuwa Wadaiwa wawili ambao majina yao yamehifadhiwa wangeendelea kupunguza deni hilo hadi pale litakapokamilika jambo ambalo inadaiwa imebakia kuwa ndoto za alinacha.               


"Mwandishi tangu mwaka jana 2023 hadi leo 2024 mawasiliano yamekatika na sina cha kufanya nimebakia kuteseka na Watoto wangu watatu na kukosa msaada wa aina yoyote.Alisema Fatuma.                            


Kufuatia kadhia hiyo Fatuma alisema changamoto anayo ipitia kwa sasa ni Mwanafunzi wa kidato cha tano anayeanza mhura huu wa June 30 aitwaye Salma Bakari Hamis kushindwa kuanza kufanya maadalizi .       



"Matokeo yametoka na amefauru kwenda shule ya Sekondari ya Wasichana Ulanga mkoani Morogoro mtoto huyu amawezaje kwenda kama siyo kurudi kuwa mzurulaji na kujiingiza kanye matukio na tabia za hovyo" ? Alihoji Fautuma.                              


"Namuomba Mhe.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu na mtetezi wetu kulibeba hili na kuona mtoto anakweba Masomoni na haki inatendeka kwa kuwabaini wote walio jihusisha na tukio la kutapeliwa kwangu na kuuzwa kwa nyumba yangu kwa stayle ya kausha damu" Alisema Fatuma.          


Aidha alisema anamuomba Mhe.Samia Suluhu Hassan Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuone anavyoweza kulifuatilia tukio hili na kubaini kiini cha utapeli huo na jinsi ambavyo Viongozi waandamizi wa hospitali ya Mkoa Kitete walivyoingia kulipa fedha hizo kiasi cha sh.milioni 4 mbele ya Viongozi wa Serikali ngazi ya mkoa .                                          



"Wanyonge tunaonewa na kudhalilishwa hasa akina mama kwa kukosa msaada kutoka kwa Viongozi wenye dhamana kwa kuwa hatuna uwezo wa kupambana na Vyombo vya kisheria na ikizingatiwa wadhurumaji hukimbilia kutumia Mawakili wasomi ili hali wengine uwezo wa kumlipa Wakili hatuna na Serikali inashindwa kutusimamia Maskini Watoto Yatima na Wajane." Alisema Fatuma.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI