TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII
NA JOSEA SINKALA.
Mbunge wa jimbo la Nkasi kaskazini (CHADEMA) Mhe. Aida Kenani, ameishauri Serikali kupunguza matumizi ya fedha kwenye miradi isiyo na ulazima au uharaka na kuelekeza fedha hizo kwenye maeneo ambayo yana hali mbaya ikiwemo ukosefu wa magari ya Jeshi la Zimamoto hapa nchini.
Hayo yamesemwa leo Alhamisi Juni 6,2024 bungeni Jijini Dodoma na Mbunge huyo wa Nkasi Kaskazini (CHADEMA) kutoka Mkoani Rukwa wakati akichangia hoja binafsi ya Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini (CCM) Mhe. Priscus Tarimo kuhusu halmashauri za miji na wilaya kushirikiana na jeshi la zimamoto na uokoaji katika kutatua tatizo la upungufu wa magari ya zimamoto pamoja na vifaa vinavyotumika kuzima moto sanjari na uokoaji.
Mbunge Aida amesema Halmashauri zenye uwezo mkubwa kiuchumi ni vema zikashirikiana na jeshi hilo kununua vitendea kazi hususani magari ya zimamoto lakini akaiangukia Serikali kwa kuendekeza matumizi yanayozidi uwezo ikiwemo kununua magari ya kifahari ya wakuu wa Wilaya wakati maeneo mengine yakiwa na upungufu ikiwemo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
“Jambo la kwanza ambalo naweza nikashauri kama jambo hili la kununua magari ya zima moto ni kipaumbele chetu tupunguze matumizi ambayo hayana ulazima. Mhe. Spika (Dkt. Tulia Ackson) tulipitisha hapa makadirio ya kununua ma DC zaidi ya milioni 400 , kipaumbele chetu kama ni magari ya zimamoto kulikuwa na sababu gani yakupeleka fedha zote hizo kwenye magari ya DC", Amesema Mbunge huyo pekee wa CHADEMA kwa mujibu wa CHADEMA.
0 Comments