Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Halmashauri ya mji wa Njombe Mkoani Njombe imepanga kujibu hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG Kabla ya Mwezi septemba mwaka huu kutokana na hoja 15 kati ya 30 kutofungwa.
Aidha Changamoto ya serikali kutumia maeneo ya Chama cha mapinduzi CCM nayo imeibua hoja kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG na kusababisha Hoja kutofungwa.
Katika mkutano wa baraza maalum la madiwani la kujadili hoja za CAG halmashauri ya mji wa Njombe licha ya kupata hati safi lakini imebainika kuwa na hoja 15 ambazo hazijafungwa jambo ambalo Mkurugenzi Kuruthum Sadick ameahidi kuzifanyika kazi kabla ya mwezi Septemba mwaka huu.
Baadhi ya madiwani akiwemo Michael Uhahula,Alatanga Nyagawa na Edwin Mwanzinga wametaka kuona namna ya kukutana na Chama ili kumaliza hoja hizo kwani changamoto hiyo ni kubwa katika maeneo mengi hapa nchini.
Awali Katibu tawala mkoa wa Njombe Judica Omary ameelekeza kuchukuliwa hatua za kufungwa kwa hoja hizo haraka na wataalamu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Njombe Mhe.Erasto Mpete amesema kutokana na ukubwa wa hoja hiyo ipo haja ya busura kubwa kutumika katika pande zote kwa chama na serikali ili kufunga hoja hizo.
Justin Nusulupila ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Njombe ambaye anasema wanasubiri ujio wa serikali ili waweze kujadiliana namna ya kufunga hoja za mali zinazoingiliana na serikali pamoja na Chama.
0 Comments