Header Ads Widget

MADADA POA NA WATEJA WAO 30 WAKAMATWA WAKIJIUZA UBUNGO

 


Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko akiwa na Timu yake wiki hii wameendelea na oparesheni ya kushtukiza katika eneo la Sinza Jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia June 15,2024 kwa lengo la kuyabaini na kuyafungia maeneo yanayotumiwa na Madada poa kuuza miili yao (Madanguro) ambapo wamefanikisha kukamatwa Watu 30 wakiwemo Madada poa 25 pamoja na Wateja wao watano.


DC Bomboko amefanya msako wa lodge kwa lodge na gesti kwa gesti kwenye nyumba zote za wageni zilizokuwa zimebadilishwa kuwa Madanguro kwa Mdada kulipa Tsh. elfu 10 kwa siku na kutumia chumba kujiuza siku nzima na Wanaume tofauti ambapo ameagiza zifungwe huku akiwataka Wamiliki wajisalimishe ofisini kwake na ameagiza pia kufungwa kwa Bar na Night Club kadhaa eneo la Sinza ambazo hutumiwa pia na Wadada hao kutafuta Wateja wa kuwauzia miili yao.

Chanzo :Habari Jamii 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI