NA WILLIUM PAUL, SAME.
MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori kutoka Shirika la uhifadi wa Mazingira na Wanyama pori Duniani (WWF) ambao wametembelea Wilayani Same wakiongozwa na Mratibu wa Southern Kenya Northern Tanzania (SOKNOT) Dk. Maurus Msuha anayesimamia shughuli za uhifadhi kwa upande wa Tanzania na Kenya.
Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa kwenye mazungumzo hayo ni pamoja na namna ya kufanya kazi kwa pamoja kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori katika Wilaya ya Same ambapo kumekuwa na changamoto ya uvamizi wa wanyama waharibifu wanaovamia kwenye mashamba ya wananchi na kuharibu mazao ikiwemo Tembo wanaotoka hifadhi ya Taifa ya Mkomazi hasa kipindi hiki cha kiangazi.
Aidha Kasilda amelishukuru Shirika la WWF kwa ushirikiano wao wanaouonesha ndani ya Wilaya ya Same, nakusisitiza kuwa ushirikiano uliopo uendelee kuduma ili kusaidia kuunga mkono jitihada za Serikali za kutatua changamoto ya migongano ya wanyamapori na binadamu.
Kwaupande wake Mratibu wa Southern Kenya Northern Tanzania SOKNOT Dk. Maurus Msuha amepongeza Serikali kwa hatua mbalimbali wanazozichukua za kukabiliana na changamoto ya uvamizi wa Wanyama hao ikiwemo uzinduzi wa bomu baridi la kufukuzia Tembo lililozinduliwa hivi karibuni kwa ngazi ya wilaya.
Mwisho..
0 Comments