NA WILLIUM PAUL, SAME.
MKUU wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni ameongoza kikao cha mapato cha Wilaya ambacho kinalenga kushauriana namna ya kuweza kufikia lengo la ukusanyaji wa mapato kwa wakati lakini pamoja na kutatua changamoto na malalamiko yanayojitokeza wakati maafisa wanapotekeleza majukumu ya msingi kisheria.
Pamoja na mambo mbalimbali yaliyojadiwa kwenye kikao hicho lakini pia ameagiza Taasisi zote zinazohusika na ukusanyaji wa mapato kuhakikisha wanatumia ubunifu, weledi na busara ili kufikia lengo waliyojiwekea.
Aidha amesisitiza pia Taaisi hizo kuendelea kufanya tafiti na operesheni za mara kwa mara ili kubaini changamoto zilizopo kwenye vyanzo vya ukusanyaji wa mapato ili wawezekuchukua hatua na kufanya kuwa endelevu kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
Kikao hicho cha mapato kinajumuisha wajumbe toka taasisi zinazokusanya mapato ikiwemo TRA, RUWASA, TFS, Halmashauri na Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.
0 Comments