Header Ads Widget

DC KASILDA ASHIRIKI UJENZI WA VYUMBA VITANO VYA MADARASA SHULE YA MSINGI MISUFINI..

 


NA WILLIUM PAUL, SAME. 


MKUU wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni ameongoza baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Misufini Same Mashariki kuchanganya zege ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa shule ya Msingi Misufini ulioibuliwa kwa lengo la kuboresha miundombinu ya awali ambayo ni chakavu.


Ujenzi wa Madarasa hayo unatekeleza na halmashauri kwa fedha Serikali kuu pamoja na Serikali ya kijiji hicho (FORCE ACOUNT) kwa gharama ya Shilingi Milioni 125 ambazo kati yake shilingi Milioni 100 fedha kutoka Serikali kuu na Milioni 25 nguvu kazi ya wananchi, ambapo umeanza Mei 21 mwaka huu na kutarajiwa kukamilika ifikapo Juni 30, 2024.



Akizungumza mara baada ya zoezi hilo Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza kuwepo na usimamizi mzuri kwa mafundi katika hatua zote za ujenzi wa majengo hayo kuwezesha kukamilika kwa wakati ili uweze kuwa na matumizi endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.


“Nimshukuru sana Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupatia fedha kuboresha miundombinu ya Elimu Msingi na Sekondari kwenye Wilaya yetu, lakini pia nimpongeze Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Anne Kilango kwa jitihada zake za kuwapambania wananchi pamoja na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo kwenye Jimbo lake.



Aidha akiwa Kijini hapo Kasilda ametembelea pia Shule ya Sekondari Misufini Goma kukagua hali ya utekelezaji wa mradi huo ambao tayari umeanza kutumiwa na wananafunzi.

Mwisho... 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI