Header Ads Widget

BREAKING:AJALI YAUA IRINGA

 


AJALI imetokea majira ya saa Moja usiku kwenye mteremko wa Ipogolo mjini huku Watu Wanne wakiwemo watoto watatu wa familia Moja wakipoteza  maisha.


Matukio Daima media imezungumza na mashuhuda wa ajali hiyo ambao wamedai chanzo ni dereva boda boda (pikipiki) ambae alikuwa akitaka kulipita Lori eneo hilo la mteremko mkali .


Ajali hiyo imetokea eneo la Kisima Cha bibi barabara kuu ya Iringa -Dodoma ambapo dereva boda boda akiwa amepakia watoto watatu alipogongana na Lori la Mizigo lenye Namba za  usajili RAG 450N.


 Mashuhuda hao wamedai kuwa watoto watatu wa familia Moja walikuwa wamepakizwa kwenye boda boda wamepoteza maisha pamoja na dereva boda boda ambao wote majina yao hayajafahamika mara Moja .


Kuwa watoto hao wakiongozwa na dada yao wa Miaka 7 walitoka mjini Iringa Kuelekea nyumbani kwao Ipogolo kwa usafiri huo wa boda boda ambao ulikuwa ukiendeshwa na Mjomba wao.


Kuwa baada ya kufika eneo la Kisima Cha bibi mwendesha bodaboda wakati akitaka kulipita gari la Mbele alimgonga mtembea kwa Miguu na kuanguka barabarani na kukanyagwa na Lori lililokuwa limebeba Makaa ya mawe Kuelekea barabara ya Dodoma.

Kuwa wote wanne akiwemo dereva walikanyagwa na Lori Hilo na kufa Papo hapo.

kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Alfred Mbena alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwa miili ya watu hao iliifadhiwa chumba Cha Maiti hospital ya rufaa ya mkoa wa Iringa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI