Header Ads Widget

ASIMWE AKUTWA AMEFARIKI BAADA YA KUCHUKULIWA NA WATU WASIOFAHAMIKA

Mtoto Asimwe Novarth enzi za uhai wake
 
Mwili wa mtoto Asimwe Novath ukipakizwa kwenye gari

xxxxxxxxx

Na Mariam Kagenda _ Kagera 

Mwili wa mtoto mwenye Ualbino  Asimwe Novath  ambaye  alichukuliwa na watu wasiofahamika  nyumbani kwao  katika kijiji cha Bulamula kata ya Kamachumu umekutwa ukiwa umetupwa kwenye karavati na kuondolewa baadhi ya viungo vyake vya mwili katika kijiji cha Marere kata ya Ruhanga wilaya ya Muleba.


Akizungumza baada ya kupatikana kwa Mwili huo katibu tawala wilaya ya Muleba Bwana Benjamini Mwikasyege amesema kuwa wamepata taarifa majira ya asubuhi kutoka kwa wasamalia wema walioona mwili huo na baada ya kufika katika eneo hilo walikuta mwili  ukiwa umetupwa kwenye Karavati na kukatwa mikono.


Amesema kuwa mwili wa mtoto huyo umepelekwa Mochwari na Jeshi la polis linaendelea na uchunguzi na baada ya uchunguzi  watazungumza na familia ya mtoto  kwa ajili ya kumstiri mtoto huyo katika Nyumba yake ya Milele.


Mtoto huyo aliyekuwa na umri wa miaka 2 na nusu alichukuliwa na watu wasio fahamika nyumbani kwao May 30 mwaka huu Majira ya saa moja jioni baada  ya watu wawili kuja kuomba msaada wa chumvi kwa mama wa mtoto huyo kisha kumkaba na kuchukua mtoto


Kwa upande wake Afisa mtendaji wa kata ya Ruhanga  Emmanuel Kaiza amesema kuwa alipigiwa simu na mwenyekiti wa kijiji cha Marere kuwa kuna mwili wa mtoto umepatikana katika kijiji hicho ukiwa umetupwa kwenye Karavati hivyo akafanya mawasiliano ngazi ya wilaya na ndugu wa Marehemu.


Amesema kuwa katika kata hiyo tukio kama hilo halijawai kutokea ambapo amewahimiza wananchi kujiepusha na vitendo vya ukatili kwani watu wenye ulemavu wa Ngozi wanatakiwa kuishi kama ilivyo kwa watu wengine .


Nao baadhi ya wananchi wa kijiji cha Marere kata ya Ruhanga wamelaani kitendo hicho na kuliomba Jeshi la polis kuwatafuta watu waliohusika na kitendo hicho ili waweze kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI