Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma
WITO Umetolewa kwa jamii ya watu wenye ulemavu kutosita kwenda kupata mafunzo ya ufundi kwani nawao wanauwezo wa kusoma na kufanya shughuli hizo za kiufundi kama watu wengine
Wito huo umetolewa jijini hapa leo,Mei 28,2024 na Mhandisi Paul Henry kutoka katika Taasisi hiyo kwenye Maonesho ya Wizara ya Ujenzi na Taasisi zake Bungeni Dodoma
Vilevile Mha. huyo amesema kuwa Taasisi hiyo inauwezo wa kufundisha na watu wenye mahitaji maalumu kwani mwaka 2019 hadi 2020 walikuwa na watu wenye ulemavu wakijifunza fani za ufundi.
"Wenye Ulemavu kwa sasa hatuna ila tuliwanao miaka ya 2019 hadi 2020 tuliwahi kufundisha watu wenye ulemavu hatujapata Ila ni wazi kuwa uwezo wa kuwafundisha tunao changamoto ipo kwa ulemavu wa macho bado hatujapata mtaalamu wa kuwafundisha, "Amesema Mha.Huyo.
Amesema katika Taasisi hiyo hawajapata mtaalamu wa kufundisha wenye ulemavu wa macho lakini wapo kwenye kuangalia namna ya kutafuta mtaalamu ili na wenye ulemavu wa macho wapate elimu ya ufundi .
Aidha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi(ICoT) imetoa wito kwa vijana wa kike nchini kupata elimu ya ufundi ili waweze kushiriki katika shughuli zinazohusiana na ujenzi kama vijana wa kiume.
Amewataka vijana wakike wote nchini kutoamini kwamba shughuli hizo ni ngumu kwamba wao hawawezi kufanya kwani wanaweza kufanya wakati mwingine kuliko hata wanaume.
"Wito wangu wanawake wote wajue shughuli zote za ujenzi wao wananafasi kubwa yakushiriki kama wanavyoshiriki mwanaume mwingine yoyote na wasiamini kwamba hizi shughuli ni ngumu kwamba wao hawawezi kufanya,wanaweza kufanya vizuri tu
Ushuhuda ni wale ambao tayari tunawafundisha wanafanya vizuri,"amesema.
Hata hivyo amesema kuwa katika Taasisi hiyo kuna kozi maalum ya stahiki ya nguvu kazi umeunda kozi maalumu zinaitwa kozi maalumu za wanawake ,vikundi vya wanawake na vijana na wenye uhitaji maalumu.
Pamoja na hayo Mha.Henry ameeleza kuwa Taasisi hiyo ipi chini ya Wizara ya ujenzi imeanzishwa na kusajiliwa na Baraza la Elimu ya ufundi stadi(NACTVET) mwaka 2021 ambapo inatoa mafunzo ya ufundi kwa ngazi ya National Technical Award(NTA)daraja la 4 hadi 6 na mafunzo ya ufundi stadi ngazi ya Vacational Education Training (VET) daraja la 1 hadi 3.
0 Comments