Header Ads Widget

WADAU TOENI USHIRIKIANO KUTENGENEZA MIFUMO SALAMA YA KUWALINDA WATOTO

Na  Matukio Daima Media ,Mbeya

WADAU mbalimbali  Jijini Mbeya wameombwa kushirikiana katika kutengeneza  mifumo salama ya utoaji  taarifa na  upatikanaji wa masuala ya watoto  wenye uhitaji na wasio na uhitaji ili waweze kutoa taarifa  bila ya hofu  kwa kuwa wanaweza kukutwa na baya lolote pindi watakapotoa taarifa ya kufanyiwa  vitendo vya ukatili.


Kauli hiyo imetolewa Mei 16,2024 na Mkuu wa idara ya Miradi wa Child Support Tanzania (CST)inayojishughulisha na elimu Jumuishi watoto wenye ulemavu Hildergade Merhab wakati wa kikao cha kamati ya miradi ya shirika hilo ambacho kilikuwa kikijadili kazi miradi ambayo imetekelezwa kwa mwaka mmoja uliopita pamoja na miradi mipya waliyonayo

Katika Taasisi hiyo.


Aidha Merhad amesema kuwa kikao hicho pia kiliangalia  masuala ya ulinzi na usalama kwa watoto lakini pia wajibu wa kamati ya miradi ambayo wamo walimu ,wakuu wa shule ,waandishi wa habari , maafisa ustawi wa jamii ,wataratibu elimu kata  pamoja wanafunzi wenye mahitaji maalum na wasio na mahitaji , dawati la jinsia  (Polisi)na katika suala la ulinzi wa watoto  kila mmoja ana nafasi yake katika kuhakikisha kunakuwa na ulinzi kuwa suala la ulinzi jumuishi kwa watoto wenye ulemavu .


“Kama Child Support Tanzania tunaomba sana wadau wetu kwa nafasi zao kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha kutengeneza mifumo salama ya utoaji taarifa na upatikanaji ili kila mmoja wetu hasa watoto wetu wenye mahitaji na wasio na mahitaji wanaweza kutoa taarifa bila kuwana hofu kuwa kunabaya linaweza kumkuta,lakini hata wale wanaotoa taarifa waweze kulindwa na wanaopokea taarifa kwa kushirikianana serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na jeshi la polisi kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa kwa watoto waliofanyiwa vitendo vya ukatili  pamoja na idara ya afya kupitia hospitali ya Rufaa ya Kanda yaMbeya kukaa na watoto hawa”amesema Mkuu huyo wa Miradi.


 “Kwa mwaka huu tumepata miradi mitatu mipya miradi ambayo  inaenda kufanywa Rukwa, Katavi na Songwe ambao unafadhiliwa na serikali ya Ujerumani kupitia cbm  lakini pia tuna mradi wa maktaba Jumuishi ambao ni mwendelezo wa miradi ya maktaba ambayo ipo mkoa wa Mbeya inayooenda kufanywa shule ya msingi Katumba (2) shule ya msingi Mbalizi one pamoja na Itiji  huu ni mwendelezo wa mradi wa mazoezi tiba ambao unaendelezwa katika shule ya Jumuishi ya Child Support Tanzania ambapo tunaenda kuangazia masuala ya mazoezi tiba kwa watoto wenye mahitaji maalum”amesema .


Damas Mwambije ni Mwenyekiti wa kamati za miradi ya Taasisi isiyokuwa  ya kiserikali ya Child Support Tanzania (CST)amesema kuwa kikao hicho hufanyika kila baada ya miezi sita ambapo kamati hiyo husimama katikati ya wanufaika wamradi  na watoa mradi wenyewe ambao ni CST na kamati husimama kwa ajili ya kuangalia kilichoandikwa kama kimetekelezwa na kuwa mpaka sasa jumla miradi miwili mikubwa ikiwemo mradi wa peleka rafiki rafiki zangu shule ambao unaendelea katika mkoa wa Mbeya ,mradi mwingine unaenda kuanza kwa mikoa ya Rukwa ,Songwe na Katavi mradi wa uhusishaji wa rasilimali kwa ajili ya Elimu jumuishi .


“Lakini huu wa peleka  marafiki zangu shule ni mradi utakaohusisha  upimaji kielimu ,afya na afya stahiki ambazo zinapaswa watoto wenye ulemavu na watoto kwa ujumla wake  waweze kuzipata ili waweze kuwa vizuri katika masomo yao na kuleta maendeleo katika nchi yao “amesema.


Mwakilishi wa Walimu wakuu katika mradi wa Child Support Tanzania  ambaye ni mkuu wa shule  ya msingi Kyela , Asheri Ayoub amesema kuwa Taasisi hiyo imekuwa ikiwafikia watoto wengi katika upimaji watoto wenye ulemavu na ukarabati na ukarabati wa miundombinu ya watoto wenye ulemavu shule ya msingi Kyela.


“Tumelenga kuwafikia watoto wengi zaidi na Mei 31 ,2024 tutakuwa na mkutano mkubwa shule ya msingi Kyela ambao utalenga wazazi wote kwa ajili ya utambuzi wa watoto wenye mahitaji maalum hili litakuwa jambo kubwa  na kipekee na itasaidia jamii kuelewa maana ya elimu jumuishi “amesema.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI