Header Ads Widget

UTEKELEZAJI WA MATAKWA YA MKATABA WA MARRAKESHI BADO UMEKUWA KULIO SUGU KWA WASIOONA ZANZIBAR

NA MATUKIO DAIMA APP 

Ni Ukweli usiopingika kuwa, Watu Wenye Ulemavu wa Uoni mara kwa mara katika maisha yao ya kila siku wamekuwa wakikabiliwa na vitendo vingi vya kubaguliwa, kutengwa, kunyanyaswa na hata kukataliwa kutokana na hali zao.


Kwa mujibu waTakwimu kutoka Umoja wa Wasioona Duniani (WBU)  zimeleza kuwa, takribani  asilimia mbili ya Watu wote Duniani ni watu wenye ulemavu  wa macho.

Takwimu hizi hazipo mbali na Takwimu za Tanzania ambapo kwa mujibu mtandao wa Jamii Forum umeeleza kuwa Udadi ya Watanzania wenye ulemavu wa Macho ni 620,000, Idadi hiyo ni sawa na 1% ya watu katika Nchi zinazoendelea na za Uchumi wa Kati.


Hapa visiwani Zanzibar kundi hili la watu wenye ulemavu wa Macho baadhi yao wamekuwa wakijikimu maisha yao ya kila siku kwa shughuli za kuombaomba kando  kando ya barabara na hata katika nyumba za ibada katika maeneo mengi ya mjini.

Hii inatokana na ukweli kuwa, licha ya utandawazi lakini bado  kundi  hili linaendelea kukabiliwa na madhila mengi ikiwemo kufungiwa, majumbani na familia zao  kwasababu wanachukuliwa kama wanazitia aibu familia hizo au hata kuwachukulia kuwa ni laana kutoka kwa mizimu.

Kuna Mikataba  mbalimbali ukiwemo mkataba wa Marrakesh ambao Tanzania umeridhia mwaka 2019 lengo kulinda haki za Watu wenye ulemavu wa uoni licha ya kwamba utekelezaji wa matakwa ya mkataba huo umekuwa mwiba kwa  Zanzibar na kuwakosesha fursa nyingi ambazo walipaswa kuzipata.

Mkataba wa Haki miliki  wa Marrakeshi  ni makataba  wa kimataifa uliopitishwa mwaka 2013 nchini Morocco na Tanzania  umeridhia na kusainiwa mkataba huu mwaka 2020 chini ya uongozi wa Rais John Pombe Maguli  ambao unatoa fursa kwa Watu wasioona kuruhusiwa  iwapo wanahitaji kazi ambazo zinalindwa na hakimiliki waweze kuzipata bila kuomba idhini kutoka kwa wenye hakimiliki au mtunzi wa kazi husika.

Hii inalazimu nchi husika ambazo zimeridhia Mkataba huo kufanya mabadiliko katika sheria zao za hakimiliki na kuingiza  mapendekezo yote ya  Mkataba huo.

Mwandishi wa Makala haya alipata fursa ya kuzungumza na Mratibu  wa Jumuiya ya Wasioona Zanzibar (ZANAB) Bw. Adil Mohammed  Ali ambapo anaeleza umuhimu wa Mkataba wa Kitamataifa wa Marrakeshi.

Mratibu wa Jumuiya ya Wasioona Zanzibar (ZANAB) Bw. Adil Mohammed Ali  anasema kuwa, Umuhimu wa makataba huo ni kutoa  fursa kwa wasioona kuweza kupata Makala,Vitabu, majarida na vitu vyote vinavyohusiana na maandishi ya wino vikawa katika hati rafiki kwa watu wasiona.

"Mkataba huu unatupatia fursa sisi kupata makala, Majarida na hata vitabu kuwa katika njia ya hati rafiki ambazo tunaweza kusoma ikiwa kwa njia ya braille, maandishi makubwa na kusikiliza kwa sauti iliyorikodiwa." amesema.

"Ukweli kuwa tunapata vikwazo vingi katika kusoma vitabu hasa Wanafunzi hawapati vile vitabu ambavyo wanaweza kusoma kulingana na hali yao, wamekuwa wakipata vitabu vya kawaida na ukiwaambia watunzi wa vitabu hivyo kuweka katika hati rafiki za Watu Wasioona wanadai kuwa ni  gharama kubwa," ameeleza.

Aidha amesema kuwa, Umuhimu wa mkataba huo unatoa fursa kwa Watu wasiioona kuweza kujiendeleza kielimu kutokana na mazingira mazuri ya wao kujifunza.

Amesema, Mapendekezo ya Mkataba huo unatoa fursa ya wao kuweza kupata habari  kwa njia fikivu kwao. 

"Ukweli kwamba, umuhimu wa mkataba huu unatoa fursa kwa sisi kuweza kufanya tafiti mbalimbali ambazo zinaweza kusaidia kundi la watu wasioona na hata taifa kwa ujumla," ameeleza.

Bw.Adili Mohammed Mratibu wa Jumuiya ya Wasioona hapa aneleza kwamba, licha ya jitihada mbalimbali ambazo walizichukua za kutoa elimu kwa Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali kwa msaada mkubwa wa Washirika wa maendeleo wakiwemo Chama cha Wasioona Sweden (SRF) na shirika la Sight Saver International (SSI) juu ya Umuhimu wa Utekelezaji wa Matakwa ya mkataba  huo bado umekwama.

"COSOTA kule Tanzania bara tayari wameingiza vifungu vya matakwa ya mkataba wa Marrakesh katika sheria ya haki miliki na tayari wanaamza kutekeleza ila hapa kwetu licha ya kutoa elimu bado hakuna chochote  kilichofanyika," ameeleza.

Ameeleza kuwa, Mwaka 2023 ZANAB ilifanya jitihada ya kuwatafuta wahusika COSOZA na hata Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuhusu rasimu ya mkataba huo lakini jitihada ziligonga mwamba kutokana na kubadilishwa kwa Wizara.

"Tulipofuatilia tuliambiwa rasimu  ipo Wizara, Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo baadae tukaambiwa ipo Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda na hapo ndipo tulipoamza kuongeza kutoa Elimu juu ya umuhimu wa mkataba huo kwa sisi tusiiona," ameeleza.

Ameongeza kuwa, wamefanikiwa kutoa elimu kwa makatibu wakuu wote ili wafahamu umuhimu wa mkataba wa huo.

"Tumezungumza na Makatibu Wakuu wote juu ya masuala haya ya Marrakeshi ili wafahamu umuhimu wake ili yaweze kufika na kujadiliwa  katika Baraza la Mapinduzi na baadae ifikishwe katika Baraza la Wawakilishi ilidhiwe na iwe sheria," amefafanua.

"Ukweli kuwa Mkataba huu hapa kwetu umekwama kwa takribani miaka minne na hatujui sababu ni zipi licha ya jitihada mbalimbali  tulizozichukua," Amefafanua.

Hata hivyo ameeleza kwamba, Mkataba wa Marrakesh unatambua na kuhimiza kuwa Mashirika ya Serikali na yale yasiyokuwa ya kiserekali kuwajibika katika kuwapatia Wasioona na wale wenye ulemavu kusoma mbadala wa mtindo wa kupata vitabu, machapisho ambayo wanaweza kutumia kupata elimu kufanya tafiti na upatikanaji wa habari kwao.

"Mkataba wa Marrakesh ni miongoni mwa mikataba ya Umoja wa Kimataifa yenye kuhitajika sana kuridhiwa na nchi na nchi yetu pia ya Zanzibar kwa manufaa ya raia wake wenye ulemavu hususan Wasioona na wale wenye ulemavu wa kusoma kwa hakika unatoa haki na fursa kwao na kuwapa vitabu na machapisho yenye mfumo fikivu kwao, Hivyo basi haki miliki na sharia zinazoisimamia hazipaswi kubagua" amefafanua. 

Bw. Adili ameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuchukuwa hatua sasa zitakazo wezesha kuridhiwa mkataba wa Marrakesh katika Baraza la Wawakilishi lijalo. 

"Sisi Wadau tutashirikiana na serikali yetu katika kufanikisha mchakato wa kuridhia mkataba wa Marrakesh na kuendeleza jitihada za kuwahamasisha uma juu ya umuhimu na faida zake kwa wananchi na Taifa kwa jumla" amesema Bw. Adili.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI