Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma
WAKATI Tanzania ikiadhimisha siku ya chai duniani lakini bado unywaji wa chai kwa watanzania ni hafifu huku wito ukitolewa kwa jamii kuwa na utamaduni wa kunywa chai kwa wingi ili kujikinga na maradhi kama vile saratani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chai Tanzania Mustapha Umande ameyesema hayo leo jijini Dodoma katika siku ya chai Duniani na kutambua mchango wa chai katika kukuza ajira na kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Amesema serikali ya Awamu ya Sita imeweka kipaumbele kuhakikisha sekta hii inakuwa kutokana na umuhimu wake hasa kiafya ambapo husaidia kupungua athari za magonjwa ikiwemo kansa.
"Miaka mitatu ya hivi karibuni zao la chai limekumbwa na changamoto ikiwemo kushuka kwa bei na kupanda Kwa gharama za uzalishaji hivyo kuathiri mwenendo wake tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita haijatuacha tudondoke imeendelea kutoa ruzuku katika mbolea na kuhamasisha kilimo cha umwagiliaji,"amesema
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Chai Tanzania Rukia Mwango amesema serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt,Samia suluhu Hassan imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha zao la chai lina simama.
Amezitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kutoa fedha kwa ajili ya kujenga Viwanda Saba vitakavyomilikiwa na wakulima wadogo, kutoa fedha kwa ajili ya kufufua mashamba ya chai ambayo yametelekezwa kwa muda mrefu.
"Serikali ya Rais Dkt,Samia haijalala inaendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha zao hili linasimama, ametoa fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Viwanda na sasa tupo katika hatua za manunuzi vitakavyomilikiwa na wakulima wadogo.
Katika hatua nyingine ametaja changamoto zinazokabili zao la chai kuwa ni propaganda za baadhi ya watu ambazo zimechangia kudhoofisha soko la ndani la chai.
Katika siku hiyo ya chai Duniani mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde serikali ambapo amesema serikali imeweka mikakati ya kuongeza uzalishaji wa zao la chai kwa kufufua mashamba yaliyotelekezwa na kujenga Viwanda Saba vya kuchakata zao hilo vitakavyomilikiwa na wakulima wadogo.
Ameeleza mkakati mwingine wa serikali kuwa ni kuhakikisha inaweka miundombinu ya Umwagiliaji katika mashamba ya chai ili Wakulima walime misimu yote.
"Tunamshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa kipaumbele katika sekta ya kilimo ikiwemo ongezeko la bajeti hadi kufikia sh. Trillion 1.2 Wizara ya kilimo tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha sekta hii ya chai inakuwa kwa kutoa ruzuku katika pembejeo za kilimo mbolea, kutoa miche na kuongeza uzalishaji wa mbegu ,"amesema .
Mwisho
0 Comments