Na Matukio Daima App
Timu ya wakaguzi wa vifaa tiba kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba -TMDA Kanda ya Kusini wamefanya ukaguzi wa vifaa tiba vikubwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini pamoja na Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara.
Akizungumza na Mwananchi mara baada ya kumaliza ukaguzi huo Mkaguzi wa Vifaa TMDA kanda ya kusini Diana Mbwilo amesema kuwa unalenga kuhakikisha kuwa vifaa tiba vinavyokuwa kwenye hospitali vinafanyakazi kwa usalama vikiwa na ubora unaotakiwa.
Amesema kuwa katika ukaguzi huo wanafatilia ubora na ufanisi wa vifaa tiba vikubwa vinavyotumika katika mahospitali makubwa ambapo wanaangalia Mashine kama XRAY, ULTRASOUND, MRI, CTSCAN.
“Unajua hii mamlaka ndio inahusika na usajili wa hivyo vifaa tunachofanya ni ukaguzi ambapo tunaona na watalaamu wanatupitisha kwenye hizo mashine ambapo tunahoji kama kuna mashine zinafanya kile kilichokusudiwa kufanya”
“Pia tuaangalia muda wa mataengenezo kinga kama yanafanyika kwenye mashine hizo kulikangana na mzabuni aliyeleta hvi vifaa tiba vikubwa vinapaswa kukaguliwa mara kwa mara ili kujua ubora wake awali tulifanya kwenye vituo vya afya na sasa tunafanya kwenye hosptli kubwa ambapo jana tumefanya katika Hospitali yetu ya kanda na leo tupo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula” amesema Mbwilo
Nae Mkaguzi wa Vifaa TMDA Kanda ya Kusini Elias Magambo amesema kuwa zoezi hilo ni muhimu kwakuwa wanaangalia ubora wa vifaa tiba.
Amesema kuwa ili wananchi wapate huduma bora tunapaswa kusimamia uingizaji wa vifaa tiba na usimamizi wa vifaa hivyo ili kuhakikisha kuwa vinafanyakazi iliyokusudiwa vinakaa katika eneo ambalo mtengenezaji ameagiza.
“Kubwa zaidi tunaangalia kama wananchi wanapata huduma bora pia tunaangalia kama matengenezo yanafanyika kwa wakati je mtengenezaji ameweka taarifa zote ili ikitokea changamoto tunaweza kumpata je alitoa mafunzo kwa watu aliowakabidhi”
“Jambo la muhimu tunataka taarifa ya kifaa husika kililetwa lini na kilifikaje na pia tunaangalia taarifa za mtu aliyekiingiza kwakuwa sisi ndio tunaoruhusu vifaa hivi kuingia ambapo tukiona ni utunzaji tutafatilia hata kwa mtengenezaji pia tunafatilia pia” amesema Magambo
MWISHO
0 Comments