Header Ads Widget

MABALOZI WA AFRIKA KUSHIRIKI MBIO MAALUM, DAR



Na Fatma Ally, Matukio DaimaApp


Katika kuelekea kuazimisha kuanzishwa kwa Umoja wa afrika (OAU) Mei 25, 1963 Adisababa nchini Ethiopia, ambapo sasa inajulikana kwa jina (AU) mabalozi wa nchi za Afrika wameandaa mbio maalum kwa ajili ya kuenzi umoja huo ambapo zitafanyika jijini Dar es Salaam Mei 18 mwaka huu. 


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Mashariki Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Ali Bujiku amesema kuwa mbio hizo ni maalum kwa ajili ya kusaidia shule zenye uhitaji maalum ikiwemo shule mbili za sekondari na msingi ambazo ni Jangwani, Pugu, uhuru mchanganyiko na Jeshi la waokovu.


Amesema kuwa, mbio hizo ni maalumu kwa ajili ya mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania hususani waafrika, ikiwa ni kukumbuka kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika (OAU) ambapo kwa sasa inajulikana kama (AU) uliokuwa na lengo la kuzikomboa nchi ambazo hazikuwa huru kwa wakati huo.


 Wanariadha wa Kitanzania ambao wameweka alama kimataifa, Juma Ikangaa, Alphonce Simbu, Filberty Bayi na wengineo watarajia kuwemo katika mbio ambazo zimepewa jina la Africa Day Marathon zinazotarajiwa kufanyika Mei, 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam.


Aidha, amesema kuwa mbio hizo zitakuwa za kilometa 5 na 15 na zitahusisha mabalozi na baadhi ya maofisa wa kibalozi na watanzania kwa ujumla.


Hata hivyo, amesema mbio hizo maalumu ni kwa ajili ya kuadhimisha miaka 61 ya kuanzishwa OAU mwaka 1963 na mwaka 2002 kubadilishwa jina na kuitwa (AU) baada ya nchi zote za Afrika kuwa huru na sasa wakiwa wanaangalia mafanikio na kupanga mikakati ya kusonga mbele na kujiletea mafanikio katika nyanja mbalimbali.


 "Nchi nyingi za Afrika zinaadhimisha siku hiyo Mei, 25 kila mwaka, kwa Tanzania tunaadhimisha Mei 18, kutokana na Mei 25, 2024 kutakuwa na ugeni wa baraza la amani na Usalama" amesema Balozi Bujiku.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI