Na Fredrick Siwale - Matukio Daima APP Mafinga.
MGOGORO kati ya Wafanyabiashara Soko kuu Mafinga na Halmashauri ya Mji Mafinga umemalizwa kisayansi na Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
Baada ya tamko ya kufungwa utepe na Wafanyabiashara kutakiwa kuondoa bidhaa zao katika vibanda 331 vilivyo kuwa na mgogoro wa mikataba kati ya Halmashauri ya Mji Mafinga na Wafanyabiashara umemalizika baada ya maridhiano ya pande mbili kufikiwa.
Tukio hilo limefanyika ndani ya ukumbi wa ofisi za Soko kuu Mafinga,ambapo katika hali ambayo haikutarajiwa Msafara wa Viongozi kutoka Mkoani ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh.Peter Serukamba uliwasili Mafinga na kuwakuta Wafanyabiashara wakiwa hawana walijualo na hatima ya vibanda na biashara zao.
Mkuu wa Mkoa aliwataka Wafanyabiashara hao kutoa mapendekezo yao jinsi wanavyotaka muafaka ufikiwe na ndipo maoni kadhaa yalipendekezwa ikiwa ni pamoja na kiwango cha wao kulipa kila mwezi kwa Halmashauri.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa ,Mwenyekiti wa Soko kuu Mafinga Kliusi Mgaya aliwaomba Wafanyabiashara kutoa maoni yao na kuridhia makubaliano ili kumaliza mgogoro huo ambao ulishaanza kuharibu hali ya hewa Kibiashara na Kisiasa kwa Wilaya nzima ya Mufindi.
Katika mapendejezo yao Wafanyabiashara walimuomba Mkuu wa Mkoa kuridhia kila Mfanyabiashara / Mjenzi wa kibanda awe analipa sh.50,000 kila mwezi kwa Halmashauri jambalo Mkuu wa Mkoa hakuweza hakuweza kukubaliana na ombi la Wafanyabiashara hao.
Mapendekezo ya RC Serukamba ni Wafanyabiashara walipe sh.80,000 kwa kila mwezi ambapo Wafanyabiashara waliendelea kuomboleza walipe sh.55,000 kisha 60,000, 65,000 na kuishia ombi la sh.70,000 ombi ambalo Mkuu wa Mkoa Mh.Serukamba alibakia na msimamo wake.
Hitimisho Mkuu wa mkoa aliwataka wakubaliane naye ili walipe sh.80,000 na kuwataka walidhie na pia walipe kila mmoja deni alilokuwa akidaiwa kwa kipindi cha miezi sita ambayo walisitishiwa na Halmashauri kulipa kutokana na mgogoro uliokuwepo.
"Tuwe wakweli haikuwa sahihi kwa Wafanyabiashara kulipa kati ya sh.6,000 na sh.9,000 kwa mwezi hii ilikuwa ni kuinyonya Serikali na kwa makubaliano haya kuanzia Jumatano mei 22 nendeni mkaanze kuingia mikataba " Alisema Mh.Serukamba na kuwapongeza Wafanyabiashara kufikia maafikiano yenye tija kwao na Halmashauri.
Baadhi ya vibanda ambavyo vilikuwa vimezungushiwa utepe ambavyo Mkuu wa Mkoa ameagiza kuanzia mei 22 vifunguliwe na " Kazi iendelee"








0 Comments