Header Ads Widget

RC HOMERA ALIA KISA MTOTO ALIYEPOTEA, AOMBA ALIYEMCHUKUA AMREJESHE.

 


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera kwa moyo wa unyenyekevu amemuomba mtu aliyemchukua  mtoto wa miaka mitano anaefahamika kwa jina la  Joyce Laison Mkongwi  anayeishi na Wazazi wake mtaa wa Isyesye kumuonea huruma mtoto huyo na kumrejesha nyumbani akiwa salama.


Akizungumza kwa masikitiko makubwa Homera amesema aliyefanya kitendo Cha kumchukua ,Mungu ampe moyo wa Imani asimdhuru na amrejeshe salama aweze kutimiza ndoto zake za kuishi na kusoma mpaka kufikia malengo yake.


Baada ya jitihada za kumtafuta mtoto huyo Kila pande bila mafanikio tangu siku aliyopotea tarehe Mei 15, serikali ya Mkoa imeingilia kati na kuomba jamii itoe ushirikiano apatikane na  mawasiliano ya Wazazi wake namba ya simu ya baba mzazi 0764198293 na namba ya simu ya mama mzazi ni 0752939259

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI