Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya Ndele Mwaselela amewataka vijana hasa wahitimu elimu ya juu katika vyuo vikuu na vya kati kujiepusha na tabia ya kubadilisha namba za simu kwani dunia ya sasa inahitaji masawaisiliano hivyo tabia ya kubadilisha namba za simu mara kwa mara inaweza kuwakosesha fursa katika maisha.
Akizungumza na Jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (SENET) ya Vyuo vikuu na vyuo vya kati Mkoa wa Mbeya Ndele Mwaselela amesema kumeibuka tabia ambayo ameiita ni ushamba kwa vijana wengi kubadilisha na namba za simu na wakati mwingine kutopokea simu hasa wenye simu za bei kubwa wanajiono wameshafanikiwa.
0 Comments