Header Ads Widget

MADABA WAITAMANI DHAHABU YA KIJANI ILIYOPO MUFINDI.


Na, Mwanahabari wetu Matukio daima App

Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wamefanya ziara ya mafunzo Wilaya ya Mufindi kujionea shughuli za upandaji miti uchakataji wa mazao ya misitu na uhifadhi wa misitu na mazingira namna gani miti inakuza uchumi kwa wananchi wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.


Akizungumza kuhusu ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Songea alisema kuwa ziara hiyo imefanyika kwa malengo matatu ambayo ni kujifunza kuhusu upandaji wa miti kuanzia hatua ya mwanzo mpaka uvunaji, uchakataji wa mazao ya misitu katika viwanda na manufaa yake, lakini pia kujifunza namna ya kukabiliana na changamoto za uendelezaji wa rasilimali za misitu kama vile kukabiliana na majanga ya moto wa misituni.


"Nitoe pongezi zangu kwa TFS kuhusu utoaji wa elimu  ya namna ya utunzaji wa miti na mazingira kwa ujumla, lakini pia tumeona manufaa mengi ikiwa ni pamoja na  makusanyo makubwa ya mapato kwa halmashauri zote mbili za Wilaya ya Mufindi na Halmashauri ya Mji Mafinga na utoaji wa ajira kwa vijana na jamii inayozunguka maeneo ya shamba zitokanazo uwepo wa mazao ya misitu", Alisema Mkuu wa Wilaya


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Mhe. Teofanes Mlelwa amesema kuwa wamejifunza mengi na kubwa zaidi ni uwepo wa kiwanda ambacho kinatumia malighafi yote ya mti ikiwa ni mabaki ya miti katika utengenezaji wa bidhaa.


"Hivyo ni imani yangu kwamba katika Halmashauri ya Madaba tutapata kiwanda kama hicho ambacho kinakusanya mabaki yote ya miti kwa ajili ya kutengenezea bidhaa mbalimbali kwa tutaendelea kuhamasisha wananchi kupanda miti kwa wingi kama tulivyoona hapa kwaajili ya kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmojana taifa kwa ujumla."Amesema Mwenyekiti Halmashauri ya Madaba



Naye Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Wino Glory Fortunatus amesema kuwa wamekuja na viongozi kutoka halmashauri lengo ikiwa ni kujifunza na kupata uzoefu juu ya manufaa yatokanayo na uhifadhi wa misitu na wamechagua Shamba la Miti Saohill kwa kuwa ndio shamba kubwa la miti ya kupandwa hivyo anaamini kuwa wataendelea kutoa ushirikiano zaidi ili kuendeleza uhifadhi katika halmashauri ya Wilaya ya Madaba.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI