Header Ads Widget

KINANA KUUNGURUMA JIJINI DODOMA

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara Abdulrahman Kinana anatarajia kuzungumza na wanachama, wa CCM na wakazi Wa Dodoma kwa ujumla katika mkutano mkubwa utakaofanyika jijini Dodoma.


Kwa mujibu wa taarifa ya chanzo cha kuaminika, mkutano huo ambao pia utahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama cha mapinduzi, utafanyika Leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete na kurushwa moja kwa moja na vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo TBC, Channel Ten, Azam TV na mitandao ya kijamii kama vile Global TV, Millard Ayo, Jambo TV nk


Taarifa hiyo ilieleza kuwa, Kinana anatarajiwa kutumia mkutano huo kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kisiasa yanayoendelea nchini.


Hii Sio Mara y Kwanza Kwa kiongozi huyo nguli wa  CCM kufanya mikutano ya Namna hiyo ili kufafanua masuala mbalimbali YA kisiasa nchini. 


Kwa mwaka Huu, Ndugu Kinana aliwahi kukutana Na wanachama Wa Dar es Salaam katika ukumbi Wa diamond jubilee tarehe..........Na kufafanua kuwa CHADEMA ndio waliovunja mazungumzo YA maridhiano  Kati ya Pande hizo mbili.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS