Header Ads Widget

KIASI CHA BILIONI 20 KUGHALIMU UJENZI TAWI LA CHUO KIKUU KAGERA


Na Shemsa Mussa,Kagera 

Kiasi cha Billion 20 kughalimu ujenzi wa Tawi la chuo kikuu cha Dar es salaam, Mkoa kagera ujenzi utakao kamilika ndani ya Miezi 18 .

Akizungumza katika Makabidhiano ya eneo la ujenzi wa tawi la  chuo hicho  Kwa Mkandarasi,Makamu Mkuu wa Chuo Prof,Boniventure Rutinwa amesema kuwa ujenzi huo utaghalimu kiasi cha Billion 20 ndani ya miezi 18.


Prof,Rutinwa amemkabidhi Eneo kwa ajili ya ujenzi wa Chuo hicho Mkandarasi kutoka china,China Jiangxi Corporation for Internation Economic and Technical  Cooperation na kumsisitiza kukamilisha ujenzi huo kwa wakati kulingana na makubalino ya Mkataba.



Kwa upande wake Mkuu wa mkoa huo Bi Hajjat Fatma Mwassa amemtaka Mkandarasi kutoa ushirikiano zaidi  kwake pindi atakapoanza ujenzi huo ili kuepukana na changamoto zinazoweza kujitokeza baadae pia ameendelea kuwashukuru wananchi wa eneo hilo kwa ushirikiano wao kila hatua kwa ajili ya ukamilifu wa Chuo hicho kikuu.


Amesema uwepo kwa Chuo hicho utaleta fulsa nyingi ndani ya Mkoa na kitakuwa Msaada Mkubwa katika Mikoa mingine na nchi jirani ,pia amewataka wananchi kuchangamkia firsa za uwekezaji katika maeneo jirani na kitakapokuwa Chuo hicho.


Nao baadhi ya wananchi wa eneo  hilo la kijiji cha itahwa wameishukuru Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan  kwa ujio wa chuo hicho na kusema kuwa wataepuka ghalama kubwa walizokuwa wakizitumia katika masomo ya watoto wao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI