Header Ads Widget

HAKUNA GARI LA ZIMAMOTO LINALOFIKA ENEO LA TUKIO BILA MAJI-KAMANDA

 


Kamanda wa kikosi cha Zima moto mkoa wa Pwani Jenifa Shirima amesema hakuna gari la zimamoto linalofika kwenye tukio la kuzima moto bila maji.


Amekanusha dhana hiyo potofu katika jamii kwa kusema kwamba sio kweli magari ya zimamoto hufika kwenye matukio ya kuzima moto bila maji wakati akitoa mada kwenye hafla ya maadhimisho ya siku ya vyombo vya habari duniani kimkoa yaliyofanyika wilayani Kibaha mkoani Pwani ambapo wadau wa habari walihudhuria maadhimisho hayo na mada mbalimbali zilitolewa.


Amesema gari la zima moto hukaa kituoni likiwalimejaa maji kulingana na ujazo wa tanki tayari kwa safari ya kwenye tukio ambapo magari hayo ujazo wake huanzia lita 2000, 5000, 7000, 10,000, 15000 na kuendelea kulingana na ukubwa wa gari husika.



“Kwa mfano gari letu la zima moto la wilayani Kibaha lina ujazo wa lita 7000 ambalo linaweza kumwaga maji hayo katika tukio la kuzima moto kwa muda wa chini ya dakika tano kwani kasi ya matumizi ya maji hutegemea ukubwa wa moto, aina ya moto na jinsi ambavyo yule anayeendesha mtambo”


“Kwanza niweke sawa haya hayaitwi magari huitwa mitambo kwahiyo unapooperati ili maji yatoke huseti kiasi cha maji kulingana na aina ya moto na ukubwa wa moto hivyo kama umeseti namba moja yatatoka kiasi cha namba moja , mbili, tatu hata tano sawa na ukubwa na aina ya moto:”


“Na tunataka kuuzima moto usisambae maeneo mengine hivyo lazima tutatoa maji kwa presha ya kiwango kikubwa yaani hata dakika tano nyingi maji yote zaidi ya lita 7000 yanakuwa yamekwisha, sasa yakiisha wakati mtu mwingine ndio anafika kwenye tukio anaona gari la zima moto linaondoka au hata alikuwepo pale ahamini kama yale maji yanaweza ndani ya muda mfupi vile”


“Ndio ile dhana wanayokuwa nayo watu wengi kwamba gari la zima moto limekuja halina maji au limekuja na maji machache jambo ambalo sio sahihi kwani hata wewe ukiweka maji katika ndoo kubwa ukayaweka kichwani yakiwa nusu ukaanza kutembea yatacheza na kumwagika ni hivyo hivyo kwenye tanki la maji la gari la zima moto ukiweka maji pungufu gari likiwa linatembea barabarani litakuwa linacheza:”



“Kwahiyo uwezekano wa gari hilo kuanguka ni mkubwa hivyo basi lazima liwe limejaa kulingana na ujazo wake na wakati wote linapokuwa limepaki kituoni linakuwa limejaa maji kulingana na ujazo wake”

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI