Na,Jusline Marco:Arusha
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Alli Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa wanahisa wa Benki ya CRDB kuelekea Mkutano mkuu wa 29 wa wanahisa 2024 utakaofanyika Mei 17 jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habri Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo Dkt.Ally Laay amesema ujio wa Dkt.Hussein Ali Mwinyi unatokana na serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinatambua na kithamini kazi zinazofanywa na benki hiyo katika kuchangia ustawi wa pamoja wa nchi.
Dkt.Ally amesema semina hiyo ni jukwaa muhimu la kutoa elimu kwa wanahisa kuhusu masuala ya uwekezaji na huduma nyingine za fedha ambapo itahusisha mada mbalimbali zitakazowasilishwa na wataalam kuhusu uwekezaji katika masoko ya mitaji pamoja na usimamizi wa mali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Abdulmajid Nsekela mkutano huo wenye kauli mbiu ya Ustawi wa Pamoja utatoa fursa kwa wanahisa kutafakari na kuangalia maendeleo ya taasisi hiyo ya fedha,kuchangia,kujadili na kutoa miongozo ya namna ya kuboresha huduma zitolewazo na benki hiyo.
Makamu Mwrnyekiti wa Bodi hiyo Prof.Neema Mori ametoa ufafanuzi wa kauli mbiu ya Mwaka huu kuwa imelenga kuangalia ni kwa namna gani wanajenga uwezo kwa wanawake na vijana kwa kuwajengea uwezo wa kifedha na kibiashara.
Ameongeza kuwa pamoja na mambo mengine kwa mwaka huu benki hiyo imekuja na ripoti maalum ambayo imelenha kuangazia masuala ya mazingira na jamii kwa ujumla.
0 Comments