Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima amesema matokeo ya utafiti wa kujua kiwango cha ukatili dhidi ya Watoto kupitia mitandao (online child abuse) wa mwaka 2022, umebainisha asilimia 67 ya watoto wa umri wa miaka 12 hadi 17 wanatumia mitandao ambapo, kati yao 4% wamefanyiwa vitendo vya ukatili na uonevu bila ya ridhaa yao.
Waziri huyo yamesemwa leo jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025
Amesema Hiyo ni kwa kuwa Matumizi ya mitandao hayawezi kuepukwa kutokana na mapinduzi ya teknolojia ya habari na
mawasiliano ambapo mitandao ni sehemu ya maisha hasa kwa kizazi kilichopo sasa.
"Mheshimiwa Spika, katika kuwalinda
watoto dhidi ya ukatili mitandaoni, Wizara ilizindua Kampeni ya Kitaifa ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto Mtandaoni tarehe 10," Amesema
Kuimarisha ushiriki na mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Maendeleo ya Taifa.
"Mheshimiwa Spika, Wizara inalo jukumu la kusimamia na kuratibu maendeleo ya mtoto pamoja na upatikanaji wa haki za msingi kwa mtoto kama zilivyoainishwa katika Mikataba ya Kimataifa, Kikanda na Kitaifa, Sera ya Maendeleo
ya Mtoto ya mwaka 2008 na Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2019,"
Na kuongeza "Mheshimiwa Spika, haki za mtoto ni pamoja na kuishi, kulindwa dhidi ya vitendo vya ukatili, kuendelezwa kupitia vipaji na elimu, kushiriki katika masuala yanayomhusu kulingana
na umri wake na kutobaguliwa kwa namna yoyote ile, " Amesema
Aidha amesema mtoto anahitaji malezi bora yenye kuzingatia haki na mahitaji yake ya msingi hasakatika kipindi cha umri wa miaka 0-8 ambapo ubongo hukua kwa 90%. ambapo Nguvu kubwa inahitajika hapa ili kuhakikisha mtoto anakua na kufikia utimilifu wake na hatimaye kuja kuwa nguvu kazi yenye tija kwa Taifa.
Hata hivyo, baadhi ya watoto
wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na malezi duni na vitendo vya ukatili kutoka kwa ndugu wa karibu, familia na jamii inayowazunguka.
Amesema kwa kushirikiana na Wizara za Kisekta imeendelea kuboresha mifumo ya kisheria ili kuimarisha ulinzi
na usalama wa mtoto kwa kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Mtoto, Sura
ya 13, Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6 na Sheria ya Makosa ya Mtandao, Sura ya 443 kwa lengo la kumlinda mtoto nje na ndani ya Mtandao.
"Mheshimiwa Spika, kupitia Bunge lako Tukufu, Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6 imefanyiwa marekebisho katika kifungu cha 127(2) kupitia Marekebisho ya Sheria mbalimbali za Sekta ya Sheria za mwaka 2023 (The Legal Sector Laws (Miscellaneous Amendments) ili kuhakikisha maslahi ya mtoto yanalindwa hasa pale anapotoa ushahidi wake mahakamani, " Amesema Dkt Gwajima.
Aidha amesema, Wizara inaendelea kurekebisha Kanuni za Vituo vya Kulea Watoto Wadogo Mchana na Watoto Wachanga za mwaka 2012, Kanuni za Makao ya Watoto za mwaka 2012, Kanuni za Uasili Watoto za mwaka 2012 na Kanuni za Malezi ya Kambo za mwaka2012 ili kuhakikisha mazingira ya malezi ya mtoto wa kitanzania ni salama kwa makuzi stahiki.
KUHUSU WALIOJIFUNGUA MTOTO NJITI
"Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais aliyoyatoa Mei Mosi, 2024 Mkoani Arusha, kuhusu waliojifungua
watoto kabla ya siku zao kutimia (njiti) kwamba, kipindi cha uangalizi maalumu wa watoto hao hakitahesabiwa kama likizo ya uzazi; Wizara inashirikiana na Wizara nyingine za kisekta kwenye kuboresha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366.
Amesema lengo la marekebisho haya ni kuweka vifungu vya kumuongezea muda mama aliyejifungua mtoto njiti ili kuweza kupata muda wa kutosha wa kumhudumia mtoto vizuri tofauti na sheria ilivyo kwa sasa.
Hata hivyo ameliomba Bunge kupitisha makadirio ya bajeti ya wizara hiyo ya Shilingi 67,905,259,000 ili kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa, Wizara kwa mwaka 2024/25.
0 Comments