NA HADIJA OMARY
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi.Zainab Telack amesema kuunganisha kwa taarifa za vyombo vya utoaji huduma ya maji ngazi ya jamii CBWSO katika ukusanyaji wa mapato kielekroniki Utasaidia kuboresha uendeshaji wa usimamizi wa skimu za maji vijijini kwa ufanisi mkubwa .
Telack ameyasema hayo alipokuwa anafunga kikao kazi cha kuziunganisha jumuiya hizo kwenye mfumo wa kielekroniki wa ukusanyaji mapato yaliyofanyika huko Manispaa ya Lindi
Amesema mfomo huo wa GePG unaojulikana kama Maji is licha ya kudhibiti upotevu wa mapato lakini pia utawasaidia watendaji wa jumuiya hizo za watumia maji kuepukana na matatizo mbalimbali ya kifedha
"Dunia tuliyonayo sasa ni ya Sayansi na Teknolojia hivyo ili tuweze kusogea na kwenda mbali lazima tukubaliane kwamba sasa mifumo ya kielekroniki ndio ambayo itatutoa tulipo kwenda mbele zaidi"
Kwa upande wake mratibu wa mafunzo hayo kutoka ofisi za RUWASA Makao makuu George Busunzu amesema moja ya sababu ya kuingiza jumuiya hiza katika mfumo wa kielekroniki ni changamoto za mifumo ya ukusanyaji wa mapato
" lakini pia tulipata hoja ya mkaguzi mkuu wa serikali ambayo tulionekana tunakusanya nje ya mfumo kwa kukusanya zaidi ya bilioni 60 katika vyombo vya watuoa huduma ngazi ya jamii"
Nae Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Lindi Mhandisi Muhibu Lubasa amesema toka wakala wa maji vijijini ulipo anzishwa mwaka 2019 hali ya upatikanaji wa maji imeongezeka kutoka asilimia 58 mwaka 2019 hadi kufikia asilimia 72 kwa mwaka 2024
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakasifu Mfumo huo utakavyokuwa na manufaa makubwa kwao
Mwisho
0 Comments