Header Ads Widget

BARABARA YA NYENGEDI-RONDO KUJENGEWA KWA KIWANGO CHA LAMI.

 


HATUA ya Serikali kupitia wakala wa Barabara za mijini na vijijini kuanza kujenga Mradi wa barabara ya Nyengedi-Mnara -Rondo yenye urefu wa km 1.15 kwa gharama ya Shilingi milioni 939,107,800.00 kwa kiwango cha lami kumeleta faraja  kwa wananchi wa vijiji hivyo.


Ujenzi wa Barabara hiyo umewekwa jiwe la msingi na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2024 Godfrey Mzava mei 27, 2024 ikiwa ni utekelezaji wa adhma ya Serikali ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara kwa halmashauri ya Mtama na hivyo kupunguza gharama za matengenezo ya kila mwaka.



Kabla ya kuweka jiwe la msingi kiongozi huyo wa Mwenge wa uhuru Kitaifa Mnzava ameeleza matumaini yake juu ya mradi huo kuwa utakamilika kwa wakati uliopangwa mwezi Oktoba Kama mkataba unavyoelekeza huku akiwahimiza Wakala wa barabara za mijini na Vijijini Tarura kusimamia vizuri ili wanachi wapate unafuu wa huduma ambazo zitategemea barabara hiyo.



Akitoa taarifa ya mradi huo Meneja wa  (TARURA)Wilaya ya Lindi Mhandisi Dawson Paschal amesema mradi  unatekelezwa naa Mkandarasi M/s.M.E & Company Limited ukiwa kwa sasa umefikia asilimia 15 ya utekelezaji na  unakwenda kukamilisha urefu wa km 7.1 ambazo zinajengwa kwa sehemu tofauti zilizokuwa korofi zaidi.


Wakazi hao wamesema barabara hiyo itakapokamikika itawasaidia kuunganisha mawasiliano kati ya wananchi wa Nyengedi na Rondo na pia kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo hususan mazao.



“Kabla ya hapo adha ilikuwa kuwa hasa kwenye kusafirisha mazao yetu kutoka mashambani lakini wajawazito walikuwa walikuwa wanateseka kufika kituo cha afya kwa sababu barabara ilikuwa korofi sana na wa mama wengine walikuwa wanajigungulia njiani “Alisema Ramadhan Selemani Nchia    Mkazi wa Kijiji cha Mkangambili -Rondo.


Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2024 ukiwa katika halmashauri ya Mtama umekimbizwa kwa umbali wa Km 204.2 ukipita katika miradi 8 ya maendeleo yenye thamani ya Bilion 2.526 .


Mwisho 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI