Header Ads Widget

ACT YATAKA UCHAGUZI MKUU UWE WA KIDEMOKRASIA

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

CHAMA cha ACT Wazalendo kimehitimisha maadhimisho ya miaka 10 ya kuzaliwa kwake mjini Kigoma  huku kikiitaka  serikali ya Raisi Samia Suluhu Hassan kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kwa kuzingatia misingi ya demokrasia na kuwaacha wananchi kuchagua viongozi wanaowataka.

 



Mwenyekiti wa chama hicho,Othman Masoud Othman ambaye ni Makamu wa kwanza wa Raisi wa Zanzibar alisema hayo katika sherehe za kitaifa za maadhimisho hayo yaliyofanyika mkoani Kigoma.

 

Masoud alisema kuwa chama cha ACT Wazalendo kimefanya kazi kubwa ya kujijenga kitaasisi na kufanikiwa kupenya kila mahali na kwamba sasa imefika wakati wa kuchukua dolla na kutangaza kuwa chama hicho kimejipanga kuhakikisha kinashinda nafasi ya uraisi Zanzibar kwenye uchaguzi wa mwaka 2025.

 

Pamoja na hivyo Mwenyekiti huyo wa ACT Wazalendo ameitaka serikali kuhakikisha inaweka tume huru ya uchaguzi na katiba mpya mambo ambayo yatawezesha kutimiza azma yao ya kushika dola ili kuwatumikia wananchi na kubadilisha hali zao za Maisha kulingana na rasilimali zilizopo.




Akizungumza katika mkutano huo Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu amesema kuwa wao kama chama miaka 10 waliyokuwa kama chama chenye usajili wa kudumu wameweza kujijenga kitaasisi na hivyo wako tayari kuchukua mamlaka ya nchi Zanzibar nah uku bara kumsimamisha Kiongozi wa Chama Mstaafu wa chama hizo, Zitto Kabwe kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

“Tunajua Mnamtaka Zitto kuwa mbunge wenu hapa mjini kwenye uchaguzi ujao lakini sisi kama chama tunataka atuvushe kwenye nafasi ya uraisi wa Tanzania kutokana na uwezo na nafasi aliyonayo na tunaomba mtoe baraka zenu kufanikisha hilo,”Alisema Jussa.




Kwa upaande wake kiongozi wa Chama Mstaafu,Zitto Kabwe.


Akizungumzia mpango wa chama kumtaka kugombea uraisi wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa 2025 alisema kuwa alijipanga kugombea ubunge jimbo la Kigoma Mjini lakini chama kinayo maamuzi na wakiamua hivyo hana kipingamizi.

 

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI