Header Ads Widget

ZIARA ZA KIMKAKATI ZA VIONGOZI WA TANZANIA ZIMEKUZA MAHUSIANO

  





Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma

KATIKA kipindi cha miaka 60 ya Muungano, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango; Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi; Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) walifanya ziara za kimkakati katika nchi mbalimbali kwa lengo la kukuza na kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na nchi hizo. 



Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk Naibu Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati akieleza mafanikio ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.


Amesema Nchi hizo ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, Zambia, Afrika Kusini, Malawi, Namibia, Misri, Ghana, Nigeria, Oman, Qatar, U.A.E, Saudi Arabia, Ufaransa, Marekani, Norway, Ubelgiji, Vatican, Uturuki, China, India na Indonesia.



Amesema Kupitia ziara hizo Tanzania imepata mafanikio mbalimbali katika maeneo ya uwekezaji, biashara, ujenzi wa miundombinu, ulinzi na usalama, masuala ya kijamii, ufadhili wa masomo na matibabu na utalii. 


Mfano, "katika ziara ya Mhe. Rais Samia nchini U.A.E Tanzania imefanikisha kusainiwa kwa Hati za Makubaliano ya Ushirikiano 37 katika sekta za mawasiliano, mafuta na gesi, kilimo, utalii wa mikutano, usafirishaji, viwanda, miundombinu zenye thani ya Dolla za Marekani takribani Billion 8 ambapo Tayari wawekezaji hao wamewasili nchini kwa ajili ya utekelezaji wa miradi husika, " Amesema


Kwa upande wa ziara nchini China, imeshuhudiwa utiaji Saini wa Mikataba na Hati za Makubaliano ya kimkakati 15. Makubaliano hayo yalilenga kuimarisha biashara na uwekezaji ambapo China imeisamehe Tanzania deni la thamni ya Shilingi bilioni 31.4, pia imeipatia Tanzania msaada wa shilingi bilioni 35.72 na mkopo wa masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 56 kwa ajili ya Ujenzi wa Uwanja wa Ndege (Terminal II) Zanzibar.


Kadhaika, kupitia ziara hiyo China imefungua masoko ya parachichi na mabondo ya samaki kutoka Tanzania.

Wakuu wa Nchi waliotembelea Tanzania katika miaka ya hivi karibun ni pamoja na: Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni; Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame; Rais wa Burundi, Mhe. Everiste Ndayishimiye; Rais wa DRC, Mhe. Felix Tshisekedi; Rais wa Msumbiji, Mhe. Fillipe Nyusi; Rais wa Zambia, Mhe. Hakainde Hichilema; Rais wa Malawi, Mhe. Lazarous Chakwera; Rais wa Poland, Mhe. Andrzej Duda; Rais wa Ujerumani, Mhe. Frank-Walter Steinmeier; Rais wa Romania, Mhe. Klaus Werner Iohannis; Rais wa Hungary, Mhe. Katalin Novak; Rais wa Indonesia, Mhe. Joko Widodo; Makamu wa Rais wa Marekani, Mhe. Kamala Harris; Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe.  Salvador Valdes Mesa; Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Abiy Ahmed na Naibu Waziri Mkuu wa China Mhe. Liu Guozhong na Rais wa Kenya, Mhe. William Ruto.


KUIMARIKA KWA USHIRIKIANO WA UWILI NA UJIRANI MWEMA



Katika kipindi hiki cha miaka 60 ya Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar, Tanzania imepata mafanikio katika sekta mbalimbali kupitia ushirikiano wa uwili na ujirani mwema baina yake na mataifa mengine.


Amesema Mafanikio haya yamepatikana kupitia ushirikiano uliopo ambao unatekelezwa kupitia taratibu maalum ikiwemo Tume za Ushirikiano wa Pamoja (Joint Permanent Comissions/ Joint Cooperation Commissions).


"Ushirikiano huu umeleta mafanikio kupitia kusainiwa Mikataba na Hati za Makubaliano (MoUs) ili kutekeleza maeneo mahsusi katika sekta mbalimbali za siasa, kiuchumi na kijamii.

Mathalan, kupitia makubaliano ya ushirikiano wa uwili umewezesha ushirikiano katika biashara baina ya Tanzania na nchi mbalimbali, " Amesema. 


Na kuongeza " Baadhi ya Nchi hizo ni pamoja na Oman, Qatar, Kuwait, Saudi Arabia, Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (U.A.E), Indonesia, India, Japan, Zambia, Kenya, Norway, Hungary, Uturuki, Ujerumani, Romania, Poland, Uholanzi, Ufaransa, Italia, Urusi, Algeria, Uganda, Afrika Kusini, Namibia, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Rwanda, Burundi, Marekani, China, Brazil na Vietnam, " Amesema Balozi huo.


Aidha amesema nchi ya Tanzania  imenufaika na kuongezeka kwa biashara na uwekezaji ambapo  bidhaa za kilimo, mifugo, matunda na mbogamboga zimepata masoko katika Nchi mbalimbali Katika sekta ya Miundombinu, ushirikiano wa uwili umewezesha utekelezaji wa miradi ya barabara, maji, reli, bandari na viwanja vya ndege nchini.


 "Mathalan, katika kipindi cha miaka 60 ya Muungano Zanzibar inanufaika na miradi ya ukarabati wa miundombinu ya maji yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 92.18 kutoka India. Vilevile, India imetoa mkopo wa masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kusambaza maji katika miji 24 ya Tanzania Bara na Zanzibar, " Amesema Balozi huyo.



Hata hivyo amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kunufaika na miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya miundombinu ya uchukuzi, maji na nishati kutoka Serikali ya Japan inayotokelezwa na JICA Tanzania. 


Aidha amesema Miradi iliyotekelezwa ni pamoja na mradi wa Development of Malindi Fish Landing Marketing wa Zanzibar wenye thamani ya takribani Tshs bilioni 19.610 uliokamilika mwaka 2023, mradi wa Improvement of Transport Capacity Jijini Dar es Salaam uliogharimu takribani bilioni 22.482 uliokamilika mwaka 2023; na mradi wa upanuzi wa barabara mpya ya Bagamoyo awamu ya pili (Kipande cha Moroco  Mwenge) chenye ukubwa wa Km. 4.3 uliogharimu takribani Tshs bilioni 81.350. 


Aidha, mradi wa usambazaji maji mjini Zanzibar uliogharimu takribani Tshs bilioni 217.3 ulioanza mwaka 2022 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2027.

Katika kuimarisha ushirikiano wa uwili Tanzania na nchi marafiki zimekuwa zikitafuta ufumbuzi wa Vikwazo Visivyo vya Forodha (NTBs) kwa lengo la kuimarisha biashara. Mathalan, kuanzia mwaka 2007 mpaka 2023 Tanzania na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimefanikiwa kuondoa zaidi ya vikwazo 309  vinavyo athiri biashara katika nchi zao.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI