Header Ads Widget

MCHUNGAJI MSIGWA :SINA MGANGO WA KUGOMBEA UENYEKITI CHADEMA TAIFA



TAZAMA HABARI VIDEO HAPA

NA MATUKIO DAIMA APP 

MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo ( CHADEMA)kanda ya Nyasa mchungaji Peter Msigwa amesema hana mpamgo na Wala hatamani  kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Chama hicho Taifa inayoongozwa na Freeman Mbowe .

"Zimekuwepo propaganda zinazoenezwa na wagombea wa nafasi ya Uenyekiti kanda ya Nyasa kuwa Mimi Msigwa najipanga kugombea Uenyekiti wa CHADEMA Taifa na Ezekiel Wenje kuwa katibu mkuu wa Chama Taifa  na wanafanya Propaganda hizi ili kuwarubuni wapiga kura kuwa Mimi Sina mpamgo wa Uenyekiti wa kanda naomba wapuuzeni Sina mpamgo wa kugombea Uenyekiti Taifa Mimi nataka tena Uenyekiti kanda ya Nyasa " alisema Mchungaji Msigwa.

Alisema kuwa utendaji kazi wa mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe na makamu wake Tundu Lissu pamoja na katibu mkuu John Mnyika ni mzuri na haoni sababu ya kutaka nafasi ya kitaifa .

Alisema kutokana na kazi kubwa aliyoifanya kama mwenyekiti wa kanda ya Nyasa Bado anatamani kufanya kazi hiyo zaidi na hivyo mpamgo wake kuendelea na nafasi ya kanda ili kufanikisha majimbo mengi zaidi kupata wabunge wa CHADEMA.

Mchungaji Msigwa ambae amepata kuwa mbunge wa Jimbo la Iringa mjini kwa vipi vipindi viwili kati ya mwaka 2010 Hadi 2020 alisema kuwa matananio yake kuona mkoa wa Mbeya ,Songwe Njombe na Iringa bunge lijalo linakuwa na sura mpya za wabunge wa CHADEMA wenye Uwezo wa kupigania maendeleo ya wananchi na sio kuwa na wabunge wa ndio Mzee .

Hivyo alisema ili CHADEMA iendele kuwa imara zaidi ni lazima wagombea wa nafasi ya Kiti Kanda wawe wenye Uwezo wa kujua changamoto za wananchi na kuzifanyia kazi sio kujisifu kwa kujuana na viongozi wakubwa serikalini ambao wameshindwa kuwatumikia wananchi.

Bila kutaja jina la mgombea alisema wapo baadhi ya wagombea wanadanganya wapiga kura kuwa wametumwa na mwenyekiti wa Chadema Taifa mheshimiwa Mbowe wagombee nafasi ya Kiti Kanda eti kwa kuwa anao Uwezo wa kumpigia simu Waziri mkuu na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan jambo ambalo si hitaji ya wananchi Wala Chama .

"Hatuhitaji kiongozi anayekuja kuongoza kwa mgongo wa Rudhiwan Kikwete ,Mwenyekiti wa CCM Taifa ama kiongozi mwingine yeyote wa Chama Cha mapinduzi huu ni Uchaguzi huu ni Uchaguzi wa ndani wa Chadema sio wa CCM sasa tusikibali kuingiza chawa ndani ya CHADEMA ambao watatuuza Mbele"

Mchungaji Msigwa  aliyasema hayo Jana nyumbani kwake Kihesa Kilolo mjini Iringa  wakati akizungumza na wanachama wa chama hicho wakiongozwa wakati wakiwapokea wanachama wa Baraza la wanawake wa Chadema (BAWACHA) mikoa ya Mbeya na Songwe waliompelekea fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti tena wa kanda ya Nyasa.

Aliwataka wajumbe wa CHADEMA  kuhakikisha wanawachagua viongozi ambao wanania ya dhati na chama hicho na siyo wale ambao wanampango wa kuhujumu Chama hicho kupitia  viongozi wa CCM ambao hawana nia njema na Chadema.

Akiongelea vipaumbele vyake iwapo atachaguliwa tena kama mwenyekiti wa chadema kanda ya Nyasa, Msigwa amesema atahakikisha anongeza idadi ya wabunge na madiwani ndani ya Kanda hiyo, pamoja na kusimamia maendeleo ya wananchi katika halmashauri zote, hivyo kuwashauri wagombea wenzake kujitafakiri upya kama wanauwezo wakuyafanya hayo, katika kanda hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya msafara wa BAWACHA kutoka Mbeya Taus Kaseke alisema kuwa wamehuzunishwa sana na kauli ya mmoja kati ya wagombea wa nafasi ya Uenyekiti kanda ya Nyasa kuwa waliomchukulia fomu Mchungaji Msigwa na mabaa medi (wahudumu wa bar) basi hao ndio watakao mpa ushindi mchungaji Msigwa na huyu akapate kura za Waimba muziki wenzake .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS