Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo ametoa maelekezo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais kuhakikisha wataalamu kwa kushirikiana na wadau wanakamilisha kanuni kanuni za usimamizi wa taka ngumu za mwaka 2009 kabla ya Bunge la bajeti kuisha.
Waziri huyo amesema hayo jijini Dodoma leo April 17,2024 katika kikao na wadau wanaozalisha bidhaa zinazofungashwa kwenye chupa za plastiki na vifungashio vya plastiki kwa lengo la kujadili njia bora ya kutokomeza uchafuzi wa mazingira kwa kutumia vifungashio hivyo.
"Katika hili niagize ofisi yangu kupitia katibu mkuu hakikisheni nataka kuona kabla ya bunge la bajeti halijaisha kanuni iwe imeshatangazwa katika gazeti la serikali na wadau mkiwa na mawazo mengine ya ziada wataalamu wapo pelekeni mawazo ya ziada vipi kuboresha eneo hili,"amesema.
Amesema serikali inaenda kupiga marufuku kabisa kuonekana kwa chupa yeyote ya plastiki mtaani hasa za rangi kwa kutengeneza kanuni hiyo ambayo itamtaka kampuni au Mfanyabishara kukusanya chupa za kampuni yake.
Ameeleza kuwa serikali inaenda kutekeleza hatua za mapitio ya kanuni za usimamizi wa taka ngumu za mwaka 2009 ambapo amesema jambo la ukusanyaji wa chupa za rangi siyo la hiari tena ni jambo la lazima hivyo amewataka wadau hao peleka meseji kwa wazalishaji wenzeo ambao hawajahudhuria kikao hicho.
Vilevile ametoa maelekezo kwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwamba baada ya kanuni hiyo wakasimamie vizuri na mzalishaji ambaye chupa yake itaonekana mtaani lazima aulizwe kwanini chupa yake ipo mtaani.
"Na hii hoja ya vifuniko ambayo Naibu Katibu mkuu amefusia hapa mkaifanyie kazi mkaangalie nini kifanyike hii mifuniko isonekane lengo kuhakikisha tunafika mahali pazuri .
"Tukitaka uwekezaji zaidi na mazingira yawe mazuri hivyo imani yangu mtajadili vizuri,vifungashio viwe vizuri,bidhaa ziuzike lakini kikubwa hapa ni kuzingatia kanuni hivyo makatibu wa kuu muandike kanuni mapema hadi wiki ijayo niwe nimeshiapata mchakato ufanyike kwenda kwenye utunzaji sahihi wa mazingira.
Hata hivyo amesema Ofisi yao imeweka utaratibu mzuri wakuona nini kifanyike na hata kwenye kanuni watajiwekea utaratibu mzuri.
"Ikiwezekana tufike wakati tuweke utaratibu leo tupo na wadau lakini ikiwezekana tuangalie Halmashauri wale ambao halmashauri zao chafu takataka zimejaa.
"Barabara nzuri lakini zimejaa takataka ikiwezekana tuwawekee kanuni katika zile zao ambazo wamejiwekea za kuzoa takataka pengine msimamizi hayupo vizuri,"amesema Dkt.Jafo.
0 Comments