Header Ads Widget

WAZAZI WAASWA KUWAPATIA WATOTO WAO ELIMU YA DINI



Na fatma Ally, Matukio Daima App, Dar


Wazazi na walezi wameshauriwa kuwapeleka watoto wao madrasa kwa ajili ya kuwajenga kiimani na kukua katika malezi mazuri ya dunia na akhera.


Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Abass Mtemvu alipokua katika mashindano ya qur an yalioandaliwa na madrasat Imaadu-Diin kwa mara ya kwanza.


Amesema kuwa, ni vyema wazazi na walezi kushirikiana pamoja katika kuwapa maadili mazuri watoto ikiwemo elimu ya dini ambayo inawafanya waishi katika malezi mazuri na bora kuwa na ufahamu hata katika masomo ya shule (elimu ya dunia).



"Elimu ya madrasa ni nzuri sana, mtoto akirudi shule mzazi anatakiwa kuhakikisha anapata muda wa kwenda madrasa, watoto wetu wasomesheni elimu zote na kwa gharama yoyote, elimu ya dini ni muhimu na elimu dunia ni muhimu pia," amesema Mtemvu.


Hata hivyo Mtemvu amewataka wazazi kuchangishana fedha za kuwalipa walimu wa Madrasa wanaofundisha watoto wao.


Ametumia fursa hiyo kuipongeza Al Madrasat Imaadu-Diin kwa kuweza kufanikisha mashindano hayo kwa mara ya kwanza lakini kwa viwango vya juu.


Aidha Mtemvu amekubali kuwa mlezi wa madrasa hiyo na kuahidi kushiriki katika kutatua changamoto zinazoikabili ikiwemo kutokuwa na Ofisi, pamoja na fedha za kuiendeshea.


Awali akisoma risala katika ufunguzi wa mashindano hayo  Hadia Khamis amesema licha ya mafanikio makubwa walioyapata tangu kuanzishwa kwa madrasa hiyo lakini wamekua wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa eneo la kujenga madrasa na msikitini hali ambayo inawafanya waumini wa dini hiyo kutembea umbali mrefu.



"Tumekua tukishiriki katika mashindano mbalimbali ikiwemo ya Afrika yalioandaliwa sheikh Nurdin Kishk na yale ya dunia yalioandaliwa na Sheikh Kaporo na kote huko wanafunzi wetu wamekua wakifanya vizuri, haya kwetu ni mashindano yetu ya kwanza na tutakua tukifanya kila mwaka"amesema Hadia. 


Aidha amesema kuwa madrasa hiyo imekua ikikosa umeme wa uhakika kwa ajili kusomea watoto nyakati za usiku hivyo kulazimika kuwaondoa mapema kinyume na malengo waliojiwekea.


Madrasa hiyo imeanzishwa ikiwa na wanafunzi wa 4 hadi sasa wamefikia  wanafunzi 120.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI