Header Ads Widget

WATOTO WATANO WAFARIKI KWA KUZAMA KWENYE DIMBWI LA MAJI

Na  Matukio Daima Media,Mbeya 

WATOTO watano wamefariki dunia mkoani Mbeya baada ya kuzama ndani ya dimbwi  la maji  wakati wakiogolea katika shamba la Kakao  lenye  ukubwa wa ekari nne katika  Kijiji cha Ngeleka kata ya  Makwale Wilaya ya Kyela mkoani hapa.


Akizungumzia tukio hilo  Kaimu Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya,Abdi Issango amesema tukio hilo limetokea April 7 ,mwaka huu  katika Kitongoji cha  Katagho Kijiji cha Ngeleka kata ya Makwale  tarafa ya  Ntebela.


Aidha Kaimu Kamanda Issango amesema kuwa watoto hao walifariki dunia wakati wakipatiwa matibabu katika zahanati ya uhai Baptist iliyopo wilayani Kyela.


"Watoto hawa walizama ndani ya dimbwi  la maji lililopo kwenye shamba la kakao lenye ukubwa wa ekari nne"amesema Kamanda Issango.


Hata hivyo Issango amewataja  Watoto walifariki kuwa ni Raphael  Mwaikale (05) mwanafunzi wa darasa la  kwanza  shule ya msingi Ngeleka,Carolina Mwamkamba (ambaye ni pacha (06) mwanafunzi wa  darasa la kwanza shule ya msingi Makwale,Lightness Kakenda (05) mwanafunzi wa chekechea shule ya msingi Ngeleka na kalebu  Mwaikombe (05) Mwanafunzi wa chekechea shule ya msingi. Ngeleka.


Akielezea zaidi Kaimu Kamanda huyo amesema Uchunguzi wa awali umebaini kuwa watoto hao walienda kuogelea kwenye dimbwi lililojaa maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha ndipo walizidiwa na maji na kuzama.


 Amesema kuwa watoto walipozidiwa maji walipiga kelele kuomba msaada wa kuokolewa na wananchi lakini tayari walikuwa katika hali mbaya na kukimbizwa katika Zahanati ya Uhai Baptist hata hivyo walifariki dunia wakiwa wanaendelea kupatiwa matibabu. 


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kutoa wito kwa wazazi na walezi kuchukua tahadhari kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa kuhakikisha wanaweka uangalizi mzuri kwa watoto wao ili kuwalinda dhidi ya maafa yatokanayo na mvua.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI