Header Ads Widget

WALEMAVU LINDI WAPEWA MAFUNZO YA USALAMA MAHALI PAKAZI

 






 WATU wenye Ulemavu kutoka katika Halmashauri tatu za Mkoa wa Lindi  wamepatiwa mafunzo  ya usalama mahali pakazi  yaliyo tolewa na   Wakala wa Usalama na Afya Mahalipakazi ( Osha) Kanda ya Kusini.

Mafunzo hayo ya siku moja yame shirikisha walemavu kutoka Wilaya za Lindi Manispaa, Kilwa na Mtama yamefanyika  katika ukumbi wa Chuo kikuu Huria uliopo Manispaa ya Lindi.

Meneja wa Osha Kanda ya Kusini Muhandisi Uswege  amesema lengo kuu la mafunzo haya ni kuwafundisha kuhusu usalama mahalipakazi, ambapo watapima afya kwa washiriki walioshiriki mafunzo hayo pamoja na vikundi vilivyopo vitapata usajili bure.

amesema wanaishukuru serikali ya Mama Samia kwa kuwawezesha  pesa kwaajili ya kutoa mafunzo ya usalama Mahlipakazi na wao kuwakumbuka watu wenye mahitaji malumu kuwapatia elimu hiyo.

"Kundi la watu wenye ulemavu ni kundi lililosahaulika hawapati hizi fursa zakupata elimu kama hii ya Usalama Mahalipakazi

Tunaishukuru serikali kwakutupatia pesa zakutuwezesha kuja kufanya mafunzo.

"Watu wenye mahitaji malumu ni makundi aliyo sahaulika kwa muda mrefu  kwamfano wenye ulemavu hawana elimu ya usalama mahalipakazi  tumewakusanya ili wapate elimu ya usalama kwao wenyewe  pia kwa jamii inayowazunguka   ndugu zao  na familia zao"

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamewashukuru Osha kwakuwapatia mafunzo pia wamesema itawasaidia kutambua usalama wao wakati wa ufanyaji wa kazi zao.

Zuhura Meza amesema  mafunzo ni mazuri pia   yatawasaidia kujua afya zao na  kuchukuwa taadhari wakati wakifanya kazi zao na kujua kama kazi wanazozifanya ni salaa .

"Tunaishukuru serikali kwa kutukumbuka sisi watu wa kusini kwa upandewangu na kwaniaba ya walemavu wenzangu natoa shukrani kwa serikali ya Mama Samia na kwa watu wa Osha  "amesema Hamadi Shaibu  mshiriki wa mafunzo .

Awali akifungua mafunzo hayo  mwakilishi wa Katibu Tawala kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Lindi Herieti Kalua  amekiri mafunzo hayo  kuwa na msaada mkubwa kwa kundi hilo ambapo aliahidi  kuyazingatia.

"Niwashukuru sana Osha kwa haya mafunzo waliyo yatoa.Niwashauri vijana kujiunga katika makundi ili serikali iweze kuwasaidia kwa ukaribu.

Wenzetu Viziwi wanachangamoto ya mawasiliano  niwashauri Serikali iongeze walimu  wa Lugha ya Alama  ili waweze kuwasaidia wenzetu wenye changamoto hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS