KIKUNDI cha Kijamii cha Kibaha Huru Fikra Huru chatoa madawati 30 kwa shule za Halmashauri ya Mji Kibaha zinazokabiliwa na upungufu wa madawati.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mussa Ndomba amelishukuru Kundi hilo ambapo madawati hayo yatasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa madawati zaidi ya 3,000 kwenye shule mbalimbali za Mji wa Kibaha na kuwataka wadau wengine kuchangia kama walivyofanya kundi hilo.
Kwa upande wake Ofisa Eimu Taaluma wa Halmashauri ya Mji Kibaha Adinani Livamba kuwa madawati hayo yatasaidia kupunguza idadi ya wanafunzi ambao hawana madawati kwa darasa la kwanza la pili na la tatu.
Naye msemaji wa Kundi hilo Hamis Mponji amesema kuwa fedha zimechangwa na watu wa ndani na nje ya Kibaha ili kuwasaidia wanafunzi waondokane na changamoto hiyo ya madawati ambapo madawati hayo yana thamani ya shilingi milioni tatu.
Kwa upande wake mmoja ya viongozi wa kundi hilo Hamad Kibwelele amesema kuwa wameamua kusaidia wanafunzi ili waondokane na adha hiyo na wataendelea kusaidia jamii kupitia kundi hilo.
Mwisho.






0 Comments