Na Fredrick Siwale - Matukio Daika App Mufindi
WAHAMIHAJI haramu hao wamekamatwa april 06 ,2024 maeneo ya Msitu wa Luganga kata ya Sao hill Tarafa ya Ifwagi katika Halmashauri ya Mji Mafinga Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.
Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACAP Allan Bukumbi alithibitisha kuwa Wahamihaji hao haramu walitelekezwa katika Mashamba ya mahindi baada ya kushushwa kwenye gari ambayo awali ilisomeka kwa namba STL 3999 aina ya Landcruiser V8 yenye rangi nyeupe ambayo dereva wake aliitelekeza kwa kufunga milango na kutokomea kusiko julikana.
SACAP Bukumbi alisema Wahamiaji hao ni raia kutika Nchini Ethiopia ambao bado wanashikiliwa kituoni hapo kwa uchunguzi na Upelelezi zaidi.
Alisema baada ya uchunguzi wa awali ilibainika kuwa gari hiyo imesajiliwa kwa namba T.803 CVW aina ya Landcruiser yenye namba za usajili nambaURJ 202 - 5001217 na injini namba IUR - FE inayomilikiwa na Said Hassan mkazi wa Tabata Dar es salaam .
Katika tukio lingine SACAP Bukumbi alisema katika Oparesheni ya misako inayoendelea Polisi iliwakamata Shafii Ngailo (40) mkazi wa Uyole Mkoani Mbeya na Neema Mwangosi (42) mkazi wa Tabata Machimbo Mkoani Dar es salaam.
Alisema Watuhumiwa hao walikamatwa kwa tuhuma za kusafirisha boksi 56 za Vipodozi vilivyopigwa marufuku vyenye viambata sumu vikiwa kwenye basi la kampuni ya Rungwe kutokea Mkoni Mbeya kwenda Dar es salaam.
Msemaji huyo wa Polisi mkoani Iringa alisema Watuhumiwa watafikishwa Mahakanani wakati wowote Upelelezi utakapo kamilika.
0 Comments