Dunia David Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa DRC Kigoma
Baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa Kigoma wakiwa kwenye mkutano na Raisi wa TCCIA
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
WAFANYABIASHARA wa mkoani Kigoma wameionya serikali kuwa kama haitatekeleza maoni wanayotoa kuhusu changamoto zinazojitokeza kuhusu biashara baina yao na nchi za maziwa makuu mpango wa serikali wa kuuifanya mkoa Kigoma kuwa kitovu cha kiuchumi hautafanikiwa.
Wafanyabiashara wameeleza hayo wakitoa maoni yao kwenye mkutano na Raisi wa Chama cha wafanyabiashara,wenye viwanda na kilimo (TCCIA), Vicent Minja aliyekuwa akifanya ziara ya siku mbili mkoani Kigoma ambapo alipata nafasi ya kukutana na wafanyabiashara hao na kuzungumzia changamoto za biashara zinazojitokeza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wanaoishi Kigoma,Dunia Devid alisema kuwa kwa sasa wafanyabiashara wanaopeleka mzigo Uvira,Lubumbashi na Kalemie wamehama kutumia bandari ya Kigoma ambapo kwa sasa wengi wanatumia bandari za Mombasa nchini Kenya na Mpulungu nchini Zambia ambako mzungu ni mrefu lakini hakuna usumbufu wa kodi na taratibu za kusafirisha mzigo.
Akizungumza katika mkutano huo Raisi wa TCCIA Tanzania,Vicent Minja alisema kuwa wanazo taarifa za kuwepo kwa changamoto nyingi kwa wafanyabiashara wanaosafirisha bidhaa Kwenda nchi za maziwa makuu zipo ambazo wanazifanyia kazi ingawa bado changamoto ni kubwa.
Minja alisema kuwa moja ya jambo ambalo wanapigania kwa sasa ni kuufanya mkoa Kigoma kuwa free zone kwenye masuala ya kodi ili bidhaa zinazouzwa hapa zisiwe zimetozwa kodi kuwezesha kuondoa changamoto zilizojitokeza jambao ambalo litawezesha kuuza bidhaa kwa wingi kwenda nchi za maziwa makuu kwa gharama ya bei ya China au nchi nyingine.
Sambamba na hilo alisema kuwa mpango wa kwanza kuelekea suala hilo ni kumuomba Raisi Samia Suluhu Hassa kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa wafanyabisahara wa nchi za maziwa makuu (Lake Tanganyika Business Summit) ambapo masuala mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara na viongozi wa nchi hizo watahudhuria na mchakato kufanikisha hilo unaendelea.
Mwisho.
0 Comments