Header Ads Widget

ASKOFU KYANDO AONYA JUU YA MMOMONYOKO WA MAADILI KWA WANAFUNZI NJOMBE




Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Askofu wa jimbo katholiki la Njombe Eusebio Kyando ameonya dhidi ya Mmomonyoko wa maadili na vitendo vya ushoga Kwa wanafunzi shuleni kwani kitu pekee kinachompeleka mtoto shule ni Masomo.


Askofu Kyando ametoa onyo hilo Akiwa katika shule mpya ya sekondari Makowo Halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe baada ya kuibariki zoezi lililoenda sambamba na kubariki gari la Wagonjwa Ambulance la kituo cha afya Makowo ambapo ametaka wanafunzi hao wa kidato cha kwanza walioanzisha shule hiyo kuzingatia masomo na sio kujiingiza kwenye vitendo viovu.

 

Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Njombe Dokta Jabir Juma anasema kazi ya serikali ni kusogeza karibu huduma kwa wananchi na ndio maana imejenga kituo cha afya na sasa imepeleka gari la wagonjwa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za Afya.



Mbunge wa Jimbo la Njombe mjini Deo Mwanyika ametaka kutunzwa kwa gari hilo na si kulitumia kinyume na Malengo huku Diwani wa kata Ya Makowo Honolatus Mgaya Akisema hatua ya serikali kuwapelekea gari hilo itasaidia  kupunguza adha walizokuwa wakipata Wananchi wake.


Valentina Mlelwa Magdalena Mkonga na Remigius Msemwa ni wakazi wa Makowo ambao wanasema kupatikana kwa gari hilo kutawapunguzia adha kubwa ambayo wamekuwa wakikumbana nayo kwa kukosa usafiri.




Kituo cha Afya Makowo Tayari kimeanza kufanya kazi baada ya kujengwa hivi karibuni kikiwa ni miongoni mwa vituo vipya vya afya vya Halmashauri ya Mji wa Njombe vilivyotumia mapato ya ndani kwa asilimia kubwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI