Na Hamida Ramadan Matukio Daima App Dodoma
VYUNGU vya miche ya miti vilivyowekwa na wadau kwenye barabara kuu ya Nyerere (Kuu straight ) kwaajili ya kupendezesha Mandhari ya jiji la Dodoma vyageuzwa kuwa Chombo cha kuhifadhia uchafu ( Dastbin)
Vyungu hivyo vilivyozungushwa na kusambazwa kwenye Barabara hiyo vimeonekana kutotunzwa wala kuthaminiwa kutokana na hali hiyo ya kuenezwa uchafu
Akiongea na Matukio Daima Blog Mwenyemiti wa Mtaa wa Tofiki Alnoor Visram amesema amekuwa akihimiza wananchi wake kuzingatia suala la usafi lakini imekuwa ni Changamoto kubwa .
Amesema nikweli vyungu hivyo vimegeuzwa vibebeo vya uchafu na hiyo yote ni kutokana na eneo au Mtaa wake kuwepo katikati ya mji ambao una watu wenye tabia tofauti na kushindwa kutii kanuni za usafi.
"Kwakweli ni aibu kubwa ukizingatia hii ndio barabara kubwa hapa mjini na tukiwa tumezungukwa na ofisi kubwa bila kusahau ofisi kuu ya Chama cha Mapinzi CCM Taifa tuyapende mazingira yetu na nitoe niiombe kuwepo na utaratibu kwa watu kama hao kukamatwa na kuadhibiwa tena adhabu kari,
Sisi kama viongozi hasa wa Mtaa hatujapewa rugu la kuwakamata moja kwa moja na kuwawajibisha wale wote wanaoonekana kutupa taka hizo lakini tungepewa nafasi hii tunaimani mazingira yangekuwa safi, "Amesema
Mwenyekiti huyo ameongeza " Nitoe wito kwa Wananchi wa jiji la Dodoma kuheshimu sheria za utunzaji wa mazingira na kila mtu au Wananchi awe askari wa manzingira ili mwenzako asiweze kutupa uchafu hovyo, " Amesema
Kutokana na hayo ameiomba Serikali kuingilia kati suala hilo kwa kutoa kalipio kali kwa wote wataobainika kutupa uchafu hovyo ikiwa ni pamoja na kuwajibisha kisheria.
Naye Jafary Mnyawi mkazi wa Dodoma Kata ya Miyuji amesema Licha ya Dodoma kuwa jiji lakini ukweli ni kwamba Dodoma ni chafu tofauti na majiji mengine hapa nchini.
"Nitoe ushauri kwa Serikali kuwepo na utaribu na sheria za kuwawajibisha wachafuzi wa mazingira wote, mtu akitupa taka akamatwe kama wanavyofanya katika mikoa ya Moshi na arusha ,Dodoma ni jiji hivyo ni lazima jiji liwe safi na kupendeza, " Amesema mkazi huyo Mnyawi
Kwa Upande wake Afisa Mazingira wa jiji la Dodoma Dickson Kimaro amezungumzia suala hilo na kusema kuwa lengo la kuwepo kwa vyungu hivyo ni kupendezesha jiji la Dodoma liwe jiji la kijani (Green city) lakini imetokea kwa baadhi ya wananchi kuvigonga usiku wakiwa wamelewa na wengine kutupa taka ndani ya vyungu hivyo.
" Tukumbuke kunausemi usemao "Tunza Mazingira yakutunze kwasababu unapotupa chupa ya plastiki ndani ya mmea tambua unakwenda kuuua kwani chupa au uchafu unaoutupa hujui ina kemikali ya aina gani hivyo kutokana na tatizo hilo tumekuwa tukikamata wanaofanya uchafu na kuwapiga faini ya shilingi 300000 na kwa wanaobainika kuvigonga vyungu hivyo wanalipa faini ya shilingi 300000 na kutengeneza na kurudisha mmea au ua kama lilivyokuwa awali, " Amesema Afisa huyo
Amesema wamekuwa wakishirikina na watu wa usalama barabarani, polisi jamii,wasimamizi wa mandhari na watu wa sheria ndogo katika kukabilina na Changamoto hiyo hasa kwa madereva wa daladala, waendesha bajaji , pikipiki na watembea kwa miguu.
Aidha ametoa wito kwa baadhi ya wafanyabishara hususani wanaokaanga Chipsi na mishikaka kuacha kutupa majivu ya moto kwenye vyombo vya kuhifadhia uchafu kwani wamekuwa wakisasabisha vyombo hivyo kuungua kutokana na material yake kuwa ya plastiki.
"Kutokana na tatizo hilo Serikali kwa kushirikiana na wadau tupo kwenye mapago wa kuhakikisha tunasambaza vyombo vya kuhifadhia uchafu vya chuma ili hata vikimwagiwa moto viweze kuhimili
Pamoja na yote hayo Serikali iliweka jitihada katika uhifadhi wa mazingira kwa kuanzisha Idara ya Mazingira mwaka 1992 ili kuhimiza uhifadhi na usimamizi wa Mazingira nchini kama ilivyohimizwa na Azimio la Rio mwaka 1992 linalozitaka nchi zote duniani kutambua uhusiano uliopo kati ya maendeleo na mazingira.
Kufuatia kuanzishwa kwa Idara ya Mazingira, Tanzania iliridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa inayohusu Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira, ambapo katika kutekeleza Azimio Rio la Mwaka 1992, Tanzania iliandaa Mpango wa Kwanza wa Taifa wa Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (National Environmental Action Plan NEAP) mwaka 1994.
Kuanzia wakati huo, Sera ya Mazingira ya mwaka 1997, Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Sura 191, Programu, Mikakati, Mipango na Miongozo mbalimbali ya kitaifa ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira imeandaliwa na kutekelezwa.
Katika utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, jumla ya Sheria Ndogo 326 zimeandaliwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mikoa ya Dodoma (15), Kilimanjaro (7), Mbeya (57), Mtwara (69), Morogoro (53), Pwani (59) na Ruvuma (66).
Aidha Kuanzia mwaka 2012 hadi sasa takribani vyeti 2812 vya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) na Vyeti 1534 vya Ukaguzi wa Mazingira vilitolewa kwa Miradi mbalimbali. Vilevile, Vyeti vya Tathmini ya Mazingira Kimkakati 17 vilitolewa kwa ajili ya kuandaa na kutekeleza Sera, Mipango na Miradi ya Kimkakati.
0 Comments