Header Ads Widget

MAJALIWA AONYA MATUMIZI YA CHA ARUSHA NA SKANKA

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

 

WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa amewaonya wakulima wa zao la dawa za kulevywa aina ya Bangi kuacha mara moja kilimo hicho na watakaokaidi kutofanya hivyo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sharia.

 

Majaliwa alitoa kauli hiyo leo wakati wa zoezi la uashaji wa mwenge wa uhuru na ukimbizaji lililozinduliwa katika viwanja vya chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo alisema kuwa, hivi karibuni kumeibuka aina nyingine ya bangi yenye kiasi kikubwa cha kilevi ijulikanayo kama cha Arusha pamoja na Skanka.

 


Alisema kuwa, aina hiyo ya bengi yenye kilevi kingi huchanganywa katika sigara ambapo watumiaji wake wanapoituma hubadilika na kuwa vichaa na kuwataka vijana wanaotumia dawa hiyo kuacha ili kunusuru maisha yao.

 

“Vijana mnahitajika katika Taifa na ndio mtakaolijenga na ndio mwelekeo wa Taifa cha Arusha na Skanka vitawapotezea mwelekeo na kulifanya Taifa hili likakosa Watanzania” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

 


Na kuongeza kuwa “ Waathirika wakubwa wa cha Arusha na skanka ni watoto na vijana wenye umri wa miaka 13 hadi 24 ambao ndio nguvu kazi ya Taifa na kwa kutambua tatizo hili serikali imeongeza kasi ya kudhibiti ambapo mikoa inayoongoza kwa biashara hii ni Mara, Morogoro, Arusha Pwani, Kagera na Mwanza”.

 

“Nitoe onyo kwa Wakulima wa zao la Bangi hatua kali zitachukuliwa kwa wote wanaojihusisha na kilimo hiki na tukiwakamata hatua kali zitachukuliwa dhidi yao”.

 


Aidha Waziri Majaliwa alisema kuwa, mbio za Mwenge mwaka huu zitaendelea kusisitiza mapambano dhidi ya Rushwa chini ya kauli mbiu ya kuzuia rushwa ni jukumu lako na kuwataka kila mmoja kutimiza wajibu wake.

 

Alisema kuwa, utafiti uliofanywa mwezi Machi mwaka 2022 Tanzania inafanya vizuri katika swala la Rushwa japo sio vizuri sana na hii ni kutokana na bado wapo walarushwa na kudai kuwa ni jukumu la kila mmoja kupambana na rushwa kwani Watanzania wanapaswa kuhudumiwa bila kulipa chochote kama Rushwa.



Majaliwa alisema kuwa, kauli mbiu ya Mwenge mwaka huu ‘Tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu’ imebeba vipaombele muhimu vya kitaifa kwa mwaka huu ambapo hutoa wito kwa Watanzania wote kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za mitaa.

 

Alisema kuwa, kauli mbiu hiyo inawakumbusha Watanzania wote wenye sifa ya kuchaguliwa na kuchagua kwenda kushiriki uchaguzi huo itakapofika Oktoba mwaka huu, na kuwakumbusha kuchagua viongozi bora kwani ni watu muhimu sana na ndio walio karibu na wananchi.

 


“Kauli hii inaweka msisitizo mkubwa kwa jamii kushirika katika swala la utunzaji wa mazingira kwani linamuhusu kila mmoja hivyo tunawajibu wa kuhakikisha Dunia inaendelea kuwa mahali salama kwa viumbe vyote kutokana na ukweli kwamba shughuli za kibinadamu ndizo zimekuwa zikisababisha uharibifu wa mazingira”.

 

Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Tabia Mwita alisema kuwa, mbio za mwenge wa Uhuru zimeendelea kudumisha uhuru, Amani, mshikamano, uzalendo na umoja wa kitaifa.

 


Tabia alisema kuwa, pia mbio hizo zimekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya wananchi kwani kupitia mbio hizo wananchi wanahamasika kubuni , kuandaa na kutekrleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika maeneo yao.

 

Aidha kupitia ujumbe wa mbio za mwenge zimekuwa zikitumika kuwaelimisha wananchi juu ya namna bora ya kupambana na maradhi, ujinga na umaskini pamoja na ubadhirifu wa miradi ya maendeleo.

 

Alisema kuwa, Mwenge wa uhuru utakimbizwa kwa siku 195, ambapo utangukuka katika mikoa 31 sawa na halmashauri 195  na kazi hiyo itafanywa na vijana sita ambao wameandaliwa kikamilifu.

 

Mwisho….

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI