Header Ads Widget

UTALINGOLO NJOMBE WAKIRI KUNUFAIKA NA FEDHA ZA SERIKALI MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA



Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Wakati Serikali ikiboresha miundombinu ya Elimu nchini inayosaidia kuongeza Tija katika sekta hiyo baadhi ya wananchi wametaka pia kuboreshwa kwa miundombinu mingine ikiwemo ya Barabara.


Katika Kata ya Utalingolo Halmashauri ya Mji wa Njombe Wananchi  wanasema kuboreshwa kwa miundombinu hiyo kunasaidia kupunguza adha  na kusaidia kupanda kwa kiwango cha Ufaulu.



Wananchi hao akiwemo Nestory Mligo na Thomas Mwang'ang'ala Wamesema kuwa katika Kipindi cha Miaka Mitatu ya Uongozi wa Rais Samia Mamlakani Kata yao Imenufaika  katika Sekta ya Elimu baada ya kuboreshwa kwa Miundombinu mbalimbali ya Elimu ndani ya Kata Hiyo ikiwemo uanzishwaji wa Shule mpya ya wavulana ya Utalingolo.


Baadhi ya Watumishi Wanaofanya kazi katika Kata Hiyo akiwemo Mwalimu Erasto Godiwe mbali na kuomba kuendelea kuboreshwa kwa miundombinu hiyo lakini wanakiri kuwapo kwa unafuu kwa sasa.



Erasto Mpete Ni Diwani wa kata ya Utalingolo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe  hapa anaeleza namna Serikali Ilivyoboresha Sekta ya Elimu katika kata yake.


Taarifa ya Idara ya Elimu mkoa wa Njombe imeeleza kuwa Shule ya Sekondari ya Wavulana Utalingolo imeshika nafasi ya Kwanza Kimkoa katika Matokeo ya Kidato Cha Pili kwa Shule za Serikali.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI