Header Ads Widget

TFS WAKABIDHI MIZINGA YA NYUKI YA KISASA 300 RUFIJI

 NA SCOLASTICA MSEWA, RUFIJI.

 

WAKIPOKEA MIZINGA HIYO WAZIRI WA TAMISEMI MOHAMED MCHENGERWA NA MKUU WA MKOA WA PWANI ABUBAKARI KUNENGE

 

WAKALA wa misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Rufiji wamekabidhi mizinga ya nyuki ya kisasa 300 kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Serikali za mitaa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa kwaajili ya vikundi vya vijana 38 vilivyoomba msaada wa mizinga hiyo.

Akikabidhi mizinga hiyo Ikwiriri Wilayani Rufiji mkoani Pwani Meneja wa TFS Wilaya ya Rufiji Francis Kiondo alisema mizinga hiyo itawasaidia vijana kujiimarisha kiuchumi.

 MENEJA TFS WILAYA YA RUFIJI FRANCIS KIONDO AKIZUNGUMZA NA WAZIRI WA TAMISEMI MOHAMED MCHENGERWA 

 

Kiondo alisema mizinga hiyo ameikabidhi kwa niaba ya Kamishina Muhifadhi TFS Prof. Do Santos Silayo amekabidhi mizinga hiyo 300 kwa Mbunge wa jimbo hilo la Rufiji iliakakabidhi kwa vikundi hivyo 38 vya vijana ambapo jumla ya vikundi 38 vilipeleka maombi ya kuomba kupewa mizinga hiyo.

Alisema katika hafla hiyo vikundi vitatu vitakabidhiwa kwaniaba ya vikundi vingine ambapo Kila kikundi kitapata mizinga ya nyuki ya kisasa kumi ambayo inauwezo wa kutoa mpaka asali kilo 20 kwa mwaka ikiwa ni katika kuwasaidia uchumi Wananchi wa jimbo hilo la Rufiji.

Kiondo alivitaja vikundi vitatu vilivyokabidhiwa mizinga hiyo kwa uwakirishi kuwa ni pamoja na Chama Cha ushirika wa vijana wajasiriamali, Ikwiriri shotern karate na kikundi cha UVCCM kwa Mpalange.

Akipokea Mizinga hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mohamed Mchengerwa ameshukuru Wizara ya Maliasili na TFS kwa mizinga hiyo kwa vikundi vya vijana wa jimbo la Rufiji na kwa ushirikiano mkubwa aliopata kutoka kwa WAKALA hao katika kipindi hiki cha mafuriko ya Mto Rufiji wilayani humo ikiwa ni pamoja na Msaada wa Boti, vyakula na maturibai.

Alisema pamoja na athari mbalimbali za mafuriko wilayani humo lakini wamekuwa wakipata neema za kupata mizinga hiyo ya nyuki ya kisasa kwaajili ya vikundi 38 vya vijana.

Naye Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alishukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mahusiano mazuri na Wadau mbalimbali ambapo mahusiano hayo yamefanya Watu mbalimbali na Wadau wengi wa Maendeleo kuleta misaada mbalimbali ya hali na Mali kwa waathirika hao wa mafuriko ya Mto Rufiji kwa Wilaya za Kibiti na Rufiji.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS