Header Ads Widget

MBOZI WAPANDA MITI 2000 KUADHIMISHA MIAKA 60 YA MUUNGANO

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo, amewataka wananchi wa Wilaya ya Mbozi Mkoani humo kujenga utamaduni wa kupanda miti ili kutunza mazingira badala ya tabia ya kupanda miti kwa matukio.

 

Mkuu wa Mkoa huyo, ameyasema hayo leo (Aprili 23, 2024) wakatia wa zoezi la upndaji miti lililofanyika katika eneo la Ilembo Kata ya Vwawa.


Mhe. Chongolo amesema wananchi wanatakiwa kupanda miti kwa dhamira, na sio kufanya kama  kazi, na inatakiwa miti ikipandwa ionekane isiwe ya kutafuta.


"Nimeambiwa Halmashauri ina lengo la kupanda miti milioni 2 kwa mwaka lakini nikisema nitembee kuhesabu miti hiyo hata elfu moja sidhani kama itafika", amesema Mkuu wa Mkoa huyo na kuongeza.



"Mimi niseme ni lazima tuanze kuutengeneza huu utamaduni tokea shuleni, tutapita kila shule tukute shule inakuwa na sehemu hifadhi ya msitu shule, maeneo yetu mengi bado yana nafasi ya kuwapa wanafunzi sehemu ya kujifunza utamaduni wa kupanda miti’’, amesisitiza Mhe. Chongolo.


Amesema kuwa wakiwapatia shule ekari tano na kuwapa maelekezo ya kuitunza kuhakikisha miti hiyo inakua na pia TFS waweke vibao kutambulisha miti hiyo kwa kutumia majina ya asili na kila mti na faida zake.


‘’Katika changamoto ya uvamizi nchi yetu ina uongozi kuanzia ngazi ya Kijiji, kuna watu wameajiriwa na Serikali na wanalipwa mishahara, kuna mtu amechaguliwa na wananchi awaongoze kwa niaba yao kwanini eneo livamiwe naye yupo maana yake hajatimiza wajibu’’, ameeleza Chongolo.


‘’Napanga siku ndani ya mwezi wa tano nitakuja kuzunguka na machifu, halafu waniambie mipaka iko wapi na waniambie hicho Kijiji ni Kijiji gani yule ambaye amepewa dhamana na Serikali lakini hajatimiza wajibu wake tutasalimia wakati huo tukikuta kuna changamoto’’, amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS